Aliyekuwa
mkewe rais mwazilishi wa Afrika Kusini Nelson Mandela na shujaa wa
ukombozi bi Winnie Madikizela-Mandela amelazwa katika hospitali moja ya
Johannesburg,baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura.
Bi Winnie Madikizela anauguza majeraha ya mgongo.
Madaktari walimfanyia upasuaji wa kwanza tarehe 8 mwezi Machi baada ya uchungu kumzidia.
Hata hivyo hali yake haikuimarika na hivyo akalazimika kufanyiwa upasuaji wa pili tarehe 14 Aprili.
Familia
yake kwa taarifa waliotuma kwa vyombo vya habari wanawashukuru wale wote
wanaoungana nao wakati huu mgumu wa ugonjwa na wanaomba haki yake ya
usiri uheshimiwe.
Habari
zinawadia juma moja tu baada ya mahakama kuu ya Afrika Kusini kumnyima
haki ya kurithi makao ya aliyekuwa rais hayati mzee Nelson Mandela.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni