Mashirika
ya msaada nchini Yemen, yameonya matokeo yanaweza kuwa mabaya sana,
iwapo makubaliano ya kusitisha mapigano, yanayoungwa mkono na Umoja wa
Mataifa, hayatotekelezwa leo kuanzia leo.
Taarifa
ya mashirika ya misaada 16 pamoja na Oxfam, Islamic Relief na Save the
Children inasema kuwa watoto 137 wanakufa kila siku, kutokana na
magonjwa yanayoweza kutibiwa.
Image copyrightEPAImage captionWaasi wa- Houthi
Mashirika
hayo yanasema, karibu watu milioni 3 wamehama makwao tangu vita vita
vinavyoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya wapiganaji waasi wa- Houthi,
kuanza mwaka mmoja uliopita.
0 maoni:
Chapisha Maoni