Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
……………………………………………………
Vituo vingi vya polisi
hasa vile vilivyopo pembezoni mwa miji vimekua vikikabiliwa na
changamoto ya uchakavu wa majengo,uhaba wa majengo pamoja na vitendea
kazi suala ambalo linapunguza kasi ya jeshi la polisi katika kupambana
na uhalifu.
Hayo yameelezwa na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake Liberatus Sabas
amesema kuwa uhaba wa majengo na vituo katika maeneo ya vijiji umekua
ukipunguza ufanisi wa kazi ya polisi katika kulinda raia na mali zao
hivyo ameitaka serikali kukarabati vituo hivyo pamoja na kuweka vitendea
kazi vya kutosha.
Akizungumza katika
uzinduzi wa kituo kipya cha polisi cha Tengeru kilichozinduliwa rasmi na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa hatua ya
kuboresha vituo vya polisi itasaidia kutatua kero za kiusalama
zinazokabili maeneo mengi mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Meru amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua baadhi
ya polisi ambao huwabambikia wananchi na kujihusisha na vitendo vya
rushwa ambavyo huwaumiza wananchi wengi
Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyezindua kituo hicho amewataka Wananchi wa kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza kila mara
Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyezindua kituo hicho amewataka Wananchi wa kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza kila mara






0 maoni:
Chapisha Maoni