Mchezo
mmoja wa Ligi Kuu ya Uingereza umeendelea usiku wa Jumatatu ambapo
Stoke City ilikuwa mwenyeji wa Tottenham Hotspur katika uwanja wake wa
nyumbani wa Britannia.
Mchezo
huo umemalizika kwa wenyeji Stoke City kumaliza mchezo huo kwa kupokea
kipigo kutoka kwa Totenham Hotspur cha goli 4-0, magoli ya Tottenham
yakifungwa na Harry Kane aliyefunga magoli mawili dk. 9 na 71 na mengine
mawili yakifungwa na Dele Alli dk. 67 na 82.
Baada
ya matokeo hayo, Tottenham imefikisha alama 68 ikiwa nyuma kwa alama
tano na viongozi wa ligi, Leicester City ambao wana alama 63, kwa upande
wa Stoke City wao wamemesalia katika nafasi ya tisa ya msimamo wakiwa
na alama 47.
0 maoni:
Chapisha Maoni