Katika hafla ya utiaji saini wa mradi huo, Zanzibar iliwakikishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Makaazi Ali Khalil Mirza, wakati Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Multi Consult kutoka Norway Oyvind Holtedahl, alisaini kwa niaba ya Serikali ya Sweden.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Makaazi Katibu Mkuu Mirza, alisema kampuni ya Multi Cionsult ilishinda zabuni hiyo kati ya kampuni 12 zilizoomba kutekeleza mradi huo.
Alieleza kuwa mradi huo utakaochukua miaka mitatu na nusu hadi kukamilika kwake, utagharimu shilingi bilioni 12.7 za Kitanzania.
Amefahamisha kuwa, miongoni mwa matumizi ya fedha hizo, ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa wizara hiyo ili kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti ili wafanye kazi zao kwa ufanisi.
Mirza alieleza kuwa, lengo la Kampuni hiyo ni kusaidia katika kulijengea uwezo Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) pamoja na Idara zake kuhusu sera ya nishati ambayo ni muhimu kwa maenedeleo ya taifa.
Naye Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Multi Consult ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na ameahidi kuwa wataitekeleza kwa ufanisi mkubwa






0 maoni:
Chapisha Maoni