00:05
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha
Maombolezo kufatia kifo cha Mbunge wa zamani wa Viti Maalum Chadema
Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiaga mwili wa
marehemu Christina Lissu Mughwai aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum
kutoka Chadema katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mwanasheria
Tundu Lissu (Mb) kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai
aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mwanasheria Tundu Lissu (Mb)
kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7
mwaka huu.
PICHA NA IKULU
0 maoni:
Chapisha Maoni