Jumatano, 13 Aprili 2016

Wahandisi Temesa wapigwa msasa

R1kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase
Ole Kujan (wa pili kushoto) akipata maelekeo juu ya ufungaji wa moja ya
mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura
Semboji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na
mafundi wa Temesa.
R2kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase
Ole Kujan(katikati) akiangalia moja ya kifaa cha kupimia umeme
kinachotumika katika mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa Temesa
yaliyofunguliwa leo.
R3Mhandisi Amani Mwanga akitoa maelekezo ya namna ya kufunga moja ya
mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na
mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
R4Baadhi ya wahandisi kutoka Temesa wakiwa katika harakati za kuchuna
na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar)
Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
R5Fundi Sanifu kutoka Temesa Mganza Juma (Katikati)akiwa makini kufunga
moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi
na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
……………………………………………………………………
Na  Raymond Mushumbusi MAELEZO
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa
ili kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.
Akifungua mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA
Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea
uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa
nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme wa
kawaida haujafika.
“Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika
maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya
wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika

0 maoni:

Chapisha Maoni