Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini
kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi
kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuweko na wafanyakazi
hewa 45 mkoani Shinyanya.
Rais Magufuli, ambaye alikuwa anaongea
baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu
Valentino Mlowola, amesema kasikitishwa sana na kauli ya Mama Malecela
ambaye bila shaka alikuwa amepata ushauri mbaya toka kwa watendaji
wake.
Amesema idadi hiyo ya wafanyakazi hewa
mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili zilikuwa
bado zinaendela kuhakikiwa.
Rais Magufuli amesema pia kwamba hadi
jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi ya 5, 507 wamebainika nchi nzima,
wengi wao wakitoka katika halmashauri.
Hivyo Rais pia ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye
katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi
na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa
kazi. Wakuu wa mikoa waliapishwa mwezi uliopita.
Katika siku hiyo Rais aliwapa
wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika Orodha ya Malipo ya
Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote
nchini, na kuwataka wakuu wa Mikoa hao wasimamie zoezi hilo kwa
ukamilifu.Vile vile Rais Magufuli alionya kuwa halmashauri yoyote
baada ya muda huo itakayokuwa na mfanyakazi hewa, mkurugenzi wake
atakuwa amejifuta kazi mwenyewe.Vilevile Rais amewaagiza mawaziri
wote kuwaeleza watendaji wao wawaondoe wafanyakazi hewa wote ndani ya
kipindi hicho cha siku 15 na kubainisha kuwa watakaoshindwa kutekeleza
agizo hilo watafukuzwa kazi kwani sheria ni msumeno.






0 maoni:
Chapisha Maoni