Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.
Charles Mwijage akizungumza na kukaribisha Ujumbu wa Wataalamu kutoka
nchini Japani katika mradi wa ushauri wa kuwekeza katika Rasirimali
watu na vitendeakazi ili kuzalisha kwa tija na ubora wa bidhaa kupitia
mradi wa KAIZEN ili kuwekeza zaidi kwa namna unavyozalisha na kufanya
kazi kwa tija, wakati wataalamu hao walipokutana na Waziri huyo
wataalamu mbalimbali wa Wizara ya Viwanda na Biashara katika kikao
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo mwishoni mwa
wiki.
Waziri Mwijage amesema wataalamu
hao wanashauri mambo mengi katika uzalishaji wa bidhaa na kilimo kama
vile kuwapa uelewa zaidi wataalamu na wajasiriamali wenyewe ili kuwekeza
katika viwanda na kilimo kwa tija na ubora ili kufikia malengo ya
kuwafanya watu kuwekeza kwa tija na ufanisi, Ukielewa namna nzuri ya
uwekezaji wenye tija na ubora utaweza kufaidika na uwekezaji wako bila
kutumia nguvu na gharama kubwa sana bila mafanikio.
Katika picha kulia ni Profesa
Tetsushi Sonobe Makamu wa rais wa Shirika la GRIPS la Japan na katikati
ni Profesa Toshio Nagase Mwakilishi wa shirika la JICA nchini
Tanzania.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Profesa Toshio Nagase Mwakilishi
wa shirika la JICA nchini Tanzania akitoa utambulisho wa ujumbe
aliofuatana nao katika mkutano huo uliofanyika katika Wizara ya Viwanda
na Biashara mwishoni mwa wiki.
Profesa Tetsushi Sonobe Makamu
wa rais wa Shirika la GRIPS la Japan akiwasilisha maelezo
ya mradi huo kwa wataalamu wa Wizara ya Viwanda na biashara.
Bw. Takao Kikuchi Mshauri Mkuu wa mradi
wa KAIZEN nchini akichangia jambo katika mkutano huo uliohudhuriwa na
wataalamu mbalimbali kutoka wizara ya viwanda na biashara na Japan.
Wataalamu mbalimbali kutoka Shirika la Maendeleo la Japan JICA na Mradi wa KAIZEN wakifuatilia mazungumza katika mkutano huo.
Wataalamu kutoka Wizara ya
Viwanda na Biashara wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu
wa Japan wakati mkutano huo ukiendelea.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.
Charles Mwijage akizungumza kwa msisitiza wakati alipokuwa akielezea
mambo mbalimbali kuhusu mradi wa KAIZEN unaoendeshwa na wataalamu kutoka
nchini Japan.






0 maoni:
Chapisha Maoni