Mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela
amewataka wananchi kutunza
mazingira ili kuendana na
mabadiliko ya tabia ya nchi
Akifungua
semina ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi iliyoandaliwa na Muadhiri wa chuo kikuu
cha kilimo sokoine [sua]kilichopo mkoani Morogoro
kwa kufadhiliwa na shirika la UNCERTAINTY
REDUCTIONIN MODELS FOR UNDERSTANDING DEVELOPMENT APLICATION[UMFULA] iliyowahusisha
wadau mbalimbali kutoka mkoa wa Iringa na Njombe, iliyofanyika Mkoani
Iringa ,alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi,Nchi imejikuta
ikikumbwa na changamoto mbalimbali kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na
kuleta athari kubwa katika jamii na Taifa kwa ujumla
Kasesela
alisema mabadilikohato yameleta athari kubwa nchini ikiwa nipamoja na mafuriko
na kubolewa nyumba baadhi ya wananchi,ambapo hali hii imesababishwa na
kutojiandaa mapema kiutafiti.
“””Nchi yetu
inatatizo kubwa la kukumbwa na majanga mbalimbali,hivyo kama tutaweza kufanya
utafiti mapema na kuwa na maandalizi ya kutoshereza
kujikinga au kuzuwia majanga halii hii
haitatokea tena
Tunapofanya
utafiti tunatakiwa tutengenze uataratibu wa kushirikiana na jamii tuanzishe
mapambano ya kupokoa mazingira yetu.
Jafet
Kashagila ni muadhiri katika chuo kikuu cha kilimo sokoine [SUA] kilichopo mkoa
Morogoro ambae ndiye muandaaji wa semina hiyo alisema kuwa lengo la kuandaa
semina kuhusu utafiti wa mabadiliko ya
tabia ya nchi ni kwaajili ya kuzalisha
takwimu mbalimbali zitakazowezeza isaidia serikali ili iweze kukabiliana na
changamoto inayoikabili kuhusu athari
zinazotokana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.
Kashagila
alisema asilimia kubwa ya shughuli zinazowafanywa na binadamu zimechangia kwa
kiasi kikubwa kuleta mabadiliko ya Tabia ya nchi kutokana na kuharibika kwa
vyanzo vya maji.
‘’’’Sisi
tunataka kufanya utafiti utakaoelezea hali Fulani ya hali ya hewa ,joto pamoja
na mvua ili kutambua uhalisia wa eneo
husika’’’’’alisema
Kwa hiyo
mradi huu wa UNCERTAINTY REDUCTIONIN MODELS FOR UNDERSTANDING DEVELOPMENT
APLICATION[UMFULA]ambao umetufadhiri kufanya utafiti wa mabadiliko ya tabia ya
nchi,tutajitahidi wadau kwa kupitia
muunganiko huu wa ushirikishwaji
utatusaidia kupata taarifa mapema na kwa wakati kuhusu mabadiliko ya hali ya
hewa na hatimae serikali kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo’’’alisema
Katika
maipango yetu tumejipanga baada ya utafiti tutatoa taarifa iwasaidie serikali
na kuleta uwelewa mzuri wa mabadiliko’’’alisema
Tutashirikishana
kuanzia mwamzo na katika kila hatua
ambayo tuatafikia taarifa kwa jamii pamoja na wadau itatolewa
na hatimae kupata matokeo sahihi’’’alisema






0 maoni:
Chapisha Maoni