Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE
wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia (TLP) ameshinda kesi ya kupinga matokeo
ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo
kupitia chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Lyatonga Mrema .
Mbatia
ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa mlalamikaji (Mrema) kuamua
kufuta shauri hilo kwa hati maalumu iliyowasilishwa katika mahakama kuu
ya Tanzania Kanda ya Moshi huku akikiri kumtambua Mbatia kama mbunge
halali wa jimbo hilo.
Mbali
na utambuzi huo Mrema pia amekanusha maelezo pamoja na ushahidi wake
aliowasilisha mahakamani hapo dhidi ya Mbatia,wananchi wa jimbo la Vunjo
pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini ambazo zilitajwa
mahakamani hapo wakati wa ushahidi wake.
Ukiwasilisha
hoja mahakamani hapo mbele ya Jaji wa mahakama kuu Lugano Mwandambo ,
upande wa mlalamikaji ukiongozwa na wakili January Mkobogho ulieleza
kuwa pande mbili katika shauri hilo wamefikia makubaliano nje ya
mahakama.
Wakili
Mkobogho aliiomba mahakama kuona makubaliano hayo ambayo yako katika
maandishi kama alama kwa mujibu wa makubalinao waliyoafikiana baada ya
kuingizwa na kupokelewa mahakamani hapo kama madai.
Alisema
kwa kuwa kesi hiyo ya uchaguzi ikiwa na maslahi mapana ya umma na kwa
kuwa mlalamikiwa wa pili na watatu waliunganishwa kwenye shauri hili kwa
mujibu wa sheria aliomba kila upande ubebe gharama zao.
Wakili
Mkobogho alieleza kuwa kutokana na pande zilizokuwa zinakwaruzana
wameamua kukaa na kumalizana wenyewe na kwamba haoni sababu za
mlalamikiwa wa pili na watatu kutokubeba gharama zao wenyewe.
Jopo
la mawakili sita wa upande wa utetezi ukiongozwa na wakili , Mohamed
Tibanyendera uliileza mahakama hiyo kwamba wanaungana na mtoa maombi kwa
maslahi ya umma na kwamba wanakubali kila upande kubeba gharama zake.






0 maoni:
Chapisha Maoni