Jumanne, 29 Machi 2016

IDADI YA VIFO AJALI YA BASI IRINGA YAFIKIA 6 MAJERUHI 36,ASAS ATOA MSAADA WA DAWA KWA MAJERUHI WOTE

IDADI YA VIFO AJALI YA BASI IRINGA YAFIKIA 6 MAJERUHI 36,ASAS ATOA MSAADA WA DAWA KWA MAJERUHI WOTE


Majeruhi  wa ajali   Bi Janeth Raia  wa Rwanda  akiwa na mtoto  Ishine Jasmin ambae  pia  Raia wa Rwanda aliyepoteza mamake  mzazi katika ajali  hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimtuliza mmoja wa majeruhi baada ya kuondokewa na mama yake mzazi kwenye ajali

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw  Richard  Kasesela  (kulia )  akiwa  na mkuu  wa mkoa  wa Iringa Bi Amina Masenza  wa  kwanza  kushoto na mwenyekiti  wa kamati ya  usalama  barabarani Bw  Salim Asas wakimsaidia mmoja kati  ya majeruhi  wa ajali hiyo Bi Sarafina Mkagasana  Rai wa  Rwanda ambae  alikuwa  mmoja kati ya majeruhi wa ajali  hiyo Bi Sarafia amempoteza  ndugu  yake Janeth Mkashena  katika ajali  hiyo

 Mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Bw  Salim Asas  akimjulia hali majeruhi  Sarafina  Mkagasana Raia wa aliyelazwa katika  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa baada  ya kupata ajali ya basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express aliyekuwa amelazwa Hospitalini hapo
Mwenyekiti wa kamati ya   usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Bw  Salim Asas kulia akiwa na mkuu  wa wilaya ya  Iringa Bw Richard Kasesela  kushoto  wakisaidia  kupakia  dawa zilizonunuliwa na kamati ya  usalama barabarani kwa ajili ya majeruhi wa ajali  ya basi
 lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express
 
WANANCHI  wa Manispaa ya  Iringa mkoa  wa Iringa washerekea Pasaka kwa kwa majonzi kufuatia vifo  vya watu  sita   waliokufa   papo  hapo akiwemo aliyekuwa mgombea uenyekiti  wa UVCCM mkoa  wa Iringa Makka Msigwa na  wengine  zaidi ya 20 kujeruhiwa  vibaya  baada  ya  basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express Kutoka  Mwanza kuja  Iringa  kupinduka  eneo la  Mteremko  wa Ipogolo  mjini  Iringa  wakati basi hilo   likielekea  kufaulisha  abiria  wa  Mbeya.



Imeelezwa   kuwa baadhi ya  abiria    waliokufa  katika  ajali   hiyo na  majeruhi   ni  wale ambao   walitakiwa   kushuka stendi kuu ya mabasi  ya mabasi  yaendaye  mikoani mjini Iringa ila dereva  wa basi aligoma   kuwashusha  stendi na  kupitiliza nao  kwenda Ipogolo    kufaulisha abiria  wa Mbeya  kwanza  ndipo arudi   kuwashusha  stendi.



Ajali   hiyo  imetokea  majira ya  saa 3 usiku wa Pasaka  baada ya  basi  hilo  kufeli  breki katika  mteremko  huo huo mkali kabla ya  kupinduka .



Wema  Zuberi  ni  mmoja kati ya majeruhi  wa ajali  hiyo aliyekuwa ametoka mkoani  Dodoma  kuelekea  Mbeya  alimweleza  mwandishi  wa habari hizi    kuwa  mwendo  wa  basi hilo  toka  amepanda  Dodoma  kuja  Iringa  haukuwa  mkali  sana   ulikuwa ni  mwendo wa kawaida .



Japo  alisema  kuwa   baada ya  kuingia  mjini  Iringa katikati ya  mji  ndipo dereva  wa basi   hilo alionyesha  kuendesha basi   hilo kwa mwendo mkali  zaidi  kiasi  cha  baadhi ya  abiria  kulalamika mwendo huo na  kutaka   kushushwa ila dereva  hakuweza  kusikia zaidi ya  kuwapuuza  abiria  hao.



“Abiria  wengi   walionyesha   kumlalamikia   dereva   huyo kwanza  kutokana na  kuwapitiliza  stendi pasipo  kuwashusha na pili mwendo  kasi ambao  alikuwa  akienda nao   ili  kufanikisha  kutufaulisha abiria  tuliokuwa   tukielekea  Mbeya “



Alisema kabla ya  kufika  eneo  hilo ambalo  basi  lilipinduka kuna kona kali na mteremko  mkali  na kilichoonekana haraka  haraka ni  dereva   kushindwa kukata  kona   hiyo baada ya Breki  kufeli   na   hivyo  kulazimika  kuhama  njia  na  kugonga kingo za  barabara  hiyo na  kupinduka .

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Bw  Richard Kasesela akizungumza na  mwandishi  wa  habari  hizi eneo la   tukio alisema  kuwa zoezi la  kuendelea  kutafuta  miili  iliyobanwa na basi  hilo imekuwa  ngumu  kutokana na kukosekana  kwa gari la kuinua  basi hilo na  tayari  amemwagiza  meneja  wa Tanesco kuleta  gari  hilo na  iwapo  dereva   hayupo  basi kuamka  na  kuendesha  mwenyewe .



Hata   hivyo  alisema  kuwa kuanzia   sasa  dawa  ya  madereva  hao  ni  kuwashughulikia kwani kama Rai imekwisha   tolewa  mara  nyingi na  bado  ajali  zinaendelea   kutokea.

Kamanda   wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa  Bw  Peter Kakamba  ambae  pia  alikuwepo  eneo la  tukio kusaidia  kuokoa majeruhi na kutoa maiti katika basi hilo  pamoja na mkuu  huyo  wa  wilaya wananchi  mbali mbali walioongozwa na askari  polisi ,alisema  kuwa  watu  watano  watu 6  wamepoteza maisha katika ajali  hiyo  huku  majeruhi ni 38 kati yao 11  wameruhusiwa Hospitali

Alisema   kuwa  jeshi la  polisi  linamshikilia  dereva wa basi hilo Kastory Mwalusako (35) mkazi  wa Mbeya ambae baada ya ajali  alijisalimisha  polisi na kuwa atafikishwa mahakamani  wakati  wowote kuanzia  sasa .

Wakati 

Wakati  huo  huo serikali ya  mkoa  wa Iringa  imeipongeza kamati ya  usalama  barabarani mkoa  wa Iringa  chini ya mwenyekiti  wake  Salim Asas kwa  kujitolea msaada wa dawa  za  kuwatibu  majeruhi  wote wa ajali ya basi   hilo.


Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Bi Amina Masenza  alitoa pongezi hizo jana baada ya  kupokea msaada wa dawa  hizo  kutoka kwa  mwenyekiti Bw  Asas kuwa  kamati hiyo  imeonyesha   upendo  mkubwa kwa  majeruhi hao  huku akitaka dawa  hizo kutumika vizuri na  kuhakikisha  zinawanufaisha  majeruhi hao.

Huku kwa upande wake  mwenyekiti wa kamati   hiyo ya usalama barabarani Bw  Asas  mbali ya  kuwapa pole  majeruhi  hao bado  aliwataka  abiria  kutoa ushirikiano kwa  jeshi la  polisi kwa  kutoa taarifa  haraka  pindi  dereva anapo  kuwa anaendesha gari  bila  kuzingatia  sheria  za usalama barabarani na  kuwa iwapo basi hilo  lingeshusha abiria  stendi yawezekana kusingetokea  madhara makubwa  hivyo kwani basi hili lilikuwa  limefika salama Iringa mjini ila dereva  aliendeleza safari ambayo kimsingi haikuwepo .

0 maoni:

Chapisha Maoni