WAKATI ikiwa imebakia siku
nne ili kuanza Bunge la kujadili na kupitisha Bajeti ya serikali ya
mwaka 2016-2017,Tayari Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Hakielimu
imewataka wabunge kuondoa itikadi zao za vyama na kuungana pamoja ili
kuishinikiza serikali kupunguza fedha za matumizi ya kawaida katika bajeti ya wizara ya elimu,
Ili fedha hizo za matumizi ya kawaida zielekezwa kwenye mipango ya Maendeleo ya elimu.
Akizungumza
na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi
Mtendaji-HakiElimu,John Kalage amesema wanawataka Wabunge kuuungana na
kuishinikiza serikali kutekeleza mpango wa miaka mitano (2015-2020)
unayoitaka bajeti ya kawaida na ya maendeleo kuwa na uwiano wa asilimia 60 na 40.
Amesema Bajeti iliyopo haikizi hali halisi ya Elimu na imechangia kurudisha maendeleo ya elimu kutokana bajeti ya elimu kuwa ndogo,
Kalage
ametolea mfano Bajeti ya Fedha ya mwaka 2015/2016 bajeti nzima ya elimu
ilikuwa Bilioni 3,887.kati ya hivyo Bajeti ya maendeleo ya sekta ya
elimu ilikuwa bilioni 604 tu sawa na (16%) ya sekta nzima,huku bajeti ya matumizi ya kawaida ikiwa ni bilioni 3,282 sawa na (84%) ya Bajeti nzima jambo analodai ni vigumu elimu yetu kukuwa.
Hata
hivyo Kalage ameonesha masikitiko yake katika Bajeti hiyo kwa kusema
licha upangaji huo wa fedha inayodaiwa kuwa ni fedha ya maendeleo katika
sekta ya elimu huelekezwa katika kugharamia mikopo ya wanafunzi wa
elimu ya juu,
“Kwa mfano Bajeti ya 2015/16 bajeti ya maendeleo ilitengwa bilioni 604,lakini nusu ya fedha hizo bilioni
306 ilitengwa kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu,hivyo bajeti ya
maendeleo ya elimu ilikuwa Bilioni 298,sasa kwa hali hii elimu yetu
haitaweza kukuwa “amesema Kalage.
Kalage
ametumia nafasi hiyo kuishauri serikali kuondoa fedha za mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu katika bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu
na badala yake amesema fedha hizo
zipangwe katika matumizi ya kawaida ,kwa madai kuwa itasaidia kutoa
picha halisi ya matumizi ya maendeleo katika sekta ya elimu.
Katika
hatua nyengine,HakiElimu pia wamewataka Wabunge kuitazama kwa umakini
dhana ya elimu bure iliotengwa na Rais John Magufuli kwa kuangalia
bajeti husika inayokwenda kutekeleza elimu bure kwa madai kuwa Bajeti
iliyopo ni ndogo kabisa na hakikizi maitaji halisi.






0 maoni:
Chapisha Maoni