Dar es Salaam: Kitendo cha kuposti picha inayomuonesha akiwa ametoboa pua na kuvaa kipini kilichofanywa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kimemfanya yamkute mazito kufuatia mashehe kumjia juu na kuwa gumzo.
Gumzo
lilianza juzikati baada ya Diamond kutupia picha kwenye akaunti yake ya
Instagram, ikimuonesha akiwa amevaa kipini, kama wafanyavyo wanawake,
kitendo kilichoamsha mjadala mkubwa kwa mashabiki na wadau mbalimbali wa
muziki wake.
Wapo
waliomuunga mkono kwa maelezo kwamba hakuna mtu anayepaswa kumuingilia
kwa sababu hayo ni maisha yake binafsi, huku wengine wakienda mbele kwa
kuwatolea mfano mastaa wengine wakubwa duniani kama Chris Brown, Wiz
Khalifa, marehemu 2Pac na wengineo kwamba nao waliwahi au wametoboa pua.
Baada ya kufuatilia sakata zima, Risasi Jumamosi liliwatafuta viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam ambayo Diamond ni muumini wake na kuwauliza kama kitendo hicho alichokifanya msanii huyo ni sahihi ambapo walimjia juu na kumshutumu vikali.
Ismail
Yahya, shehe wa msikiti mmoja maarufu Kijitonyama, alisema:
“Anachokifanya huyu bwana ni upotofu na kinyume na sheria za dini ya
Kiislam. Ni makosa kwa mwanaume kutoga pua, kuvaa kipini, hereni, mikufu
au kujichora tatuu. Sasa huyu bwana kafanya yote kaona haitoshi, kaamua
na kuvaa kipini kabisa, ni makosa makubwa na kinyume na mafundisho ya
dini.”
“Astaghafirullah!
Anachokifanya huyu msanii ni makosa makubwa na kinyume kabisa na dini
ya Kiislam. Atakuwa anafanya makusudi huyu kwa sababu naamini alisoma
madrasa na alifundishwa kijana wa Kiislamu anavyotakiwa kuwa, iweje leo
ajifananishe na mwanamke? Ni makosa makubwa kwa mwanaume wa Kiislam
kutoboa pua,” alisema Ally Moshi, Shehe wa Madrasatul Nuur jijini Dar es
Salaam.
Hata
hivyo, meneja wa msanii huyo, Salam Sharaf alibuka baadaye kwenye
mitandao ya kijamii na kumtetea Diamond kuwa picha hiyo si halisi bali
ilitengenezwa.






0 maoni:
Chapisha Maoni