Posted by Esta Malibiche on JAN 13,2017
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Mshauri wa Rais masuala ya Utamaduni Mhe,Chimbeni
Kheir Chimbeni jana alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa
Baraza la Wawakilishi alipohudhuria katika Taarab rasmi ya kusherehekea
Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa
pili kushoto) Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid
Ali Juma (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi(kulia) na
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe,Kasim Majaliwa Majaliwa (wa pili kulia)
pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la
Wawakilishi katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi
ya Zanzibar iliyofanyika jana.
Wake wa
Viongozi wakuu wa Nchi wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la
Wawakilishi katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi
ya Zanzibar iliyofanyika jana iliyopigwa na Kikundi cha Taifa.
Baadhi ya
Viongozi na Waalikwa mbali mbali wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa
Baraza la Wawakilishi katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya
Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana iliyopigwa na Kikundi cha Taifa.
Kikundi
cha Taifa cha Muziki wa Taarab kikitumbuiza kwa Wimbo unaosema “Khofu
yako Iondoke”ilyoimbwa na Profesa Moahmed Ilyas katika sherehe za Taarab
rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika
jana,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu,] 13/01/2017.
0 maoni:
Chapisha Maoni