Na Ofisa habari Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeendelea kustawi katika
sekta ya elimu ambapo tathimini ya matokeo ya darasa la saba
ya Halmshauri hiyo yanaonesha kupanda kutoka asilimia 80.39 mwaka
2015 hadi asilimia 84.90% mapema mwaka jana, ikiwa ni sawa na
ongezeko la asilimia 4.51.
Akisoma taarifa wakati wa kikao cha tathimini
ambacho huwakutanisha wakuu wa shule zote za msingi na maaofisa elimu kata,
Ofisa elimu taaluma wa Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi MRIAMU NGALA
amebainisha, kuwa tathimini ya ufaulu huo umejumuisha shule 143, watahiniwa
elfu 05 mianne 38 ambapo wavulana ni elfu 02 miatatu 84 na wasichana ni elfu 03
na 54 huku wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya
Sekondari wakiwa ni elfu 460 sawa na asilimia 84.9.
Bi. NGALA ameainisha masomo ambayo
wanafunzi wamefanya vizuri zaidi kuwa ni pamoja na somo la Kiswahili
ambalo ufaulu wake ni asilimia 90. 51, Sayansi 90.13, Maarifa
87.88, Hisabati 56.34 huku somo la Kingereza likishika nafasi ya tano kwa
asilimia 27.20
Aidha, afisa elimu huyo mwenye dhamana
ya taaluma, ametaja baadhi ya malengo ambayo walijiwekea na ndiyo yaliyochangia
kufikia mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kufaulisha kwa asilimia 95,
ufuatiliaji wa utendaji kazi, uwepo wa kambi za masomo, udhibiti wa utoro wa
Wanafunzi na Waalimu, ukamilishaji wa mada kwa wakati na uwepo wa mazoezi ya
kujipima.
Idara ya elimu msingi ya Halmashauri ya
Wilaya ya Mufindi imeweka uratibu wa kufanya tathimini ya kina kwa kila mwaka
mara baada ya kutoka kwa matokeo ya mitihani ya darasa la saba ili kuangazia
mafanikio ya ufaulu kwa kila shule, kubainisha changamoto na kuziwekea mikakati
ya kuzikabili huku tathimini hiyo ikienda sanjari na kutunuku zawadi na vyeti
kwa wakuu wa shule na maofisa ilimu kata walifaulisha wanafunzi wengi zaidi
hivyo kupandisha wastani wa ufaulu wa halmashauri.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni