Posted by Esta Malibiche on JAN 26,2017 IN NEWS
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na
wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, watendaji wa kata, tarafa
pamoja na wakuu wa idara wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhusu
utekelezaji wa kodi ya majengo kwa vijiji wakati wa kikao cha kazi
kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Iringa jana.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Mahuninga, Kata ya Mahuninga wilayani Iringa, mkoani
Iringa Lonjino Mkwele akimuuliza swali Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard
Kasesela (hayupo pichani) kuhusu utekelezaji wa kodi ya majengo kwa
vijiji wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa
Halmashauri ya Iringa jana.
Mkutano ukiendelelea katika ukumvbi wa siasa ni kilimo,uliowahusisha viongozi wa serikali ya vijiji,watendaji wa vijiji,wantendaji wa kata kata,tarafa pamoja na wakuu wa Idara wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa.
VIONGOZI
wa vijiji vyote wa Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa waagizwa kusoma
mapato na matumizi ili kuwarahisishia wananchi kufahamu jinsi fedha zao
zinavyotumika na kutoa fursa kwa wananchi kupata nafasi ya kuhoji ili
kujiridhisha pale wanapokuwa na mashaka.
Agizo
hilo limetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa (DC), Richard
Kasesela wakati wa mkutano na wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji,
watendaji wa kata, tarafa pamoja na wakuu wa idara wa halmashauri ya
Wilaya ya Iringa .
Kikao
hicho cha kazi kililenga kuwakumbusha wenyeviti na watendaji wa vijiji
na Kata kutambua majukumu yao na kuyapatia majibu sawia pamoja na swala
zima la ukusanyaji mapato .
DC
Kasesela ameagiza kufanyanyika uchunguzi ili kubaini kama kuna
watendaji waliohamishwa kazi na wanatuhumiwa kuhujumu mapato ya serikali
na michango ya wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo kurudishwa
haraka.
Mkuu
huyo wa Wilaya amewaagiza watumishi wote wa serikali ngazi ya
Vitongoji, Vijiji na Kata kufanya kazi kwa haki, Usawa na uwazi na
kiwashirikisha wananchi katika kila jambo linalohusu vipaombele vya
maeneo yao.
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi wa vijiji waliohudhuria katika mkutano
huo wamempongeza mkuu wa Wilaya ya Iringa kwa kufanya mkutano uliyolenga
kuwakumbusha majukumu yao pamoja na kuwakutanisha kwa pamoja.
Wakati
huohuo, watendaji wa vijiji, watendaji wa kati pamoja na watu wa mapato
wamekumbushwa kukusanya kodi ikiwemo kodi ya majengo.
Hata
hivyo baadhi ya viongozi wa vijiji wamekuwa na wasiwasi kuhusu
utekelezaji wa kodi ya majengo kwa kusema wananchi wengi katika maeneo
hawana uelewa juu ya kodi hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahuninga, Kata ya Mahuninga wilayani Iringa, Lonjino Mkwele alitaka kujua Kodi ya Majengo itatozwaje.
Kwa
upande wake, Mdhamini wa Wilaya ya Iringa, John Brayson aliwaomba
wananchi wote kulipa kodi ya majengo kwa maendeleo ya uchumi.
Alisema
wameanza zoezi kwa kuthamini na ukusanyaji wa kodi ya majengo na
mchakataji wa taarifa za majengo umeanza katika jumla ya vijiji 133 vya
wilaya pamoja na kata 28.
Brayson
alisema kuwa wanapata changamoto katika kutekeleza sheria ya kodi ya
majengo hasa maeneo ya vijiji hapo awali walikuwa hawatozwi.
ADHABU KWA ATAKAYESHINDWA KULIPA KODI YA MAJENGO
· Kutozwa faini ya asilimia 50 ya kodi yake.
Asipolipa halmashauri imepewa mamlaka ya kukamata mali yenye thamni sawa na kodi na kuuza kufidia kodi hiyo.
Kodi
ya majengo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilianza kutozwa
mwaka 1983, katika kipindi hicho kodi hii ilitozwa katika maeneo ya
majiji, manispaa, miji midogo na makao makuu ya halmashauri ya wilaya
tu.
Lakini
mwaka 2015 yalifanyika marekebisho ya sheria kuruhusu hata maeneo
mengine ya halmashauri ya wilaya kutoza kodi ya majengo kwa kuthamini
majengo kwa njia ya mkupuo.
0 maoni:
Chapisha Maoni