Posted by Esta Malibiche on JAN 17,2017 IN NEWS
Mbunge
wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega,( kulia)akimueleza jambo Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani( kushoto) wakati wa
ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Mkuranga katika
kijiji cha Njopeka.
Na Zuena Msuya, Pwani
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema Wilaya za
Mkuranga, Rufiji pamoja na Kibiti mkoani Pwani zitaunganishwa katika
Gridi ya Taifa wakati wa kuanza kwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa
Mradi Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).
Dkt.
Kalemani alisema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua
maendeleo na utekelezaji Mradi wa Umeme Vijiji katika Wilaya hizo
pamoja na kuzungumza na wananchi.
Alifafanua
kuwa ni lazima Wilaya hizo zikaungwanishwa katika Gridi ya Taifa ili
waweze kupata umeme mwingi, wa kutosha na wa uhakika ili kuongeza kasi
na ufanisi katika shughuli za wananchi za kujipatia maendeleo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, (aliyesimama),
akizungumza na Wakazi wa Rufiji wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa
Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijiji (REA) katika
wilaya hiyo.
dkt.
kalemani aliweka wazi kuwa wakati wa kutekeleza awamu ya tatu ya mradi
wa rea, tanesco itajenga kituo kikubwa cha kupokea na kupoza umeme
katika Wilaya ya Mkuranga ili kusambaza katika Wilaya hizo.
"
Umeme unaopatikana hapa Mkuranga , Kibiti na Rufiji kwa sasa
hautoshelezi mahitaji ya watumiaji,ni mdogo sana na unakatika mara kwa
mara,kwa kuwa shughuli za kiuchumi zimeongezeka, sasa suluhu ya tatizo
hili ni kuunganisha Wilaya hizi katika Gridi ya Taifa mara tu baada ya
REA, Awamu ya Tatu kuanza", alisema Dkt. Kalemani.
Aidha
alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa huduma ya umeme kwa sasa ni
jambo la lazima kwa kila mtanzania ili kurahisisha maendeleo, hivyo ni
vyema kila mmoja ajiunganishe na huduma hiyo kupitia Mradi wa REA ambao
huduma hiyo hupatikana kwa bei nafuu na Serikali imeugharamia kwa
asilimia mia moja kwa ajili wananchi wa vijijini.
Mbunge
wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, akizungumza na wakazi wa rufiji
(hawapo pichani)wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt Medard Kalemani ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Rufiji.
Katika
hatua nyingine, aliwagiza wakandarasi wote wanaotekeleza Mradi wa Umeme
Vijijini Awamu ya Pili, katika Mkoa wa Pwani,kuwasha umeme katika
vijiji vyote ambavyo vimepitiwa na kuunganishwa na mradi wa huo ifikapo
mwishoni mwa mwezi huu wa Januari kabla ya kuaza kwa Awamu ya Tatu ya
Mradi huo.
Pia
alimuagiza Meneja Tanesco wa Mkoa huo kusimamia wakandarasi hao ili
kutekeleza agizo hilo, na endapo halitatekelezwa kama alivyoagiza hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
"Mwishoni
mwa mwezi huu nataka kuona vijiji vyote vilivyounganishwa na REA
vinawashwa umeme, nawaagiza wakandarasi wote kutekeleza agizo hilo,
Meneja Tanesco fuatiliwa na hakikisha jambo hili linatekelezwa kwa
wakati, bila kufanya hivyo mtakuwa mmejifukuza kazi mwenyewe, kwa kuwa
hakuna sababu ya kutotekeleza hili agizo", alisisitiza Dkt. Kalemani.
Sambamba
na hilo aliiagiza Tanesco,kusogeza huduma zao karibu na wateja kwa
kuweka madawati ama kujenga vituo vidogo vya huduma kwa wateja katika
kila kijiji kwa lengo la kuwafikia wananchi kwa urahisi badala ya
wananchi kuwafuata Tanesco maofisini.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, (aliyesimama
kushoto), akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga
wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na
Wakala wa Nishati Vijiji (REA) katika wilaya hiyo.
Pia
alitumia ziara hiyo kuwaeleza wananchi kuwa Serikali kupitia Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco),imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 68.5 kwa
ajili ya kuwalipa fidia, jumla ya wananchi 2913 waliopisha Mradi wa
msongo mkubwa wa umeme kutoka Somanga hadi Kinyerezi katika vijiji
vilivyopitiwa na mradi huo.
Vilevile
alibainisha kuwa fidia hiyo italipwa kwa ratiba maaalum ili kuondoa
usumbufu kwa wananchi, ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi Bilioni 42,
zimelipwa kwa wananchi 923, huku zoezi la ulipaji likiendelea kwa mujibu
wa ratiba na linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka
huu.
Awamu
ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na REA
kwa kushirikiana na TANESCO unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu(
Januari)mwaka huu, na utatekelezwa kwa takribani kipindi cha miaka
minne.
Wakazi
wa Rufiji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard
Kalemani (hayupopichani) alipokuwa akizungumza wakati wa ziara ya
kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati
Vijiji (REA) katika wilaya hiyo.
Wakazi
wa Kijiji cha Ikwiriri wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dkt. Medard Kalemani( aliyenyoosha mkono katikati) wakati wa
ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini wilayani Rufiji.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, (jukwaani kushoto) na
mbunge wa Kibiti, Ally Ungando( kulia) akizungumza na Wakazi wa Kijiji
cha Jaribu Mpakani wilayani Kibiti, mkoani Pwani wakati wa ziara yake
ya kukagua Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati
Vijiji (REA) katika wilaya hiyo. Wananchi hao wanadai fidia baada ya
kupisha mradi wa kupitisha msongo mkubwa wa umeme kutoka Somanga hadi
Kinyerezi jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni