Posted by Esta Malibiche on JAN 28,2017 IN NEWS
Nicomed Bohai ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kusaidia Sekta Binafsi
ya Kilimo Taifa (PASS)Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wakulima wakipata maelekezo katika Pass katika maonyesho ya zana za kilimo
yaliyofanyika Jijini Arusha na kumalizaika jana maonesho hayo yalikuwa ya siku mbili.Picha na Vero Ignatus Blog.
yaliyofanyika Jijini Arusha na kumalizaika jana maonesho hayo yalikuwa ya siku mbili.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo (Pass)imewataka wakulima na wajasiriamali wote
wa kilimo ,uvuvi na wafugaji wafikirie namna ya shughuli zao kitaalam.
wa kilimo ,uvuvi na wafugaji wafikirie namna ya shughuli zao kitaalam.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Nicomed
Bohai ya kwamba wakulima wafikirie kufanya shughuli zao kibiashara,watafute elimu na maarifa ili waweze kudhaminiwa kupata mkopo wa kuendeleza shughuli zao.
Bohai ya kwamba wakulima wafikirie kufanya shughuli zao kibiashara,watafute elimu na maarifa ili waweze kudhaminiwa kupata mkopo wa kuendeleza shughuli zao.
Amesema
kuwa wanajenga mahusiano ya kibiashara kutoka kwa wafanya biashara
wakubwa kwenda kwa wadogo,ili wale ambao wameshapiga hatua wawainue wale
ambao bado,kwa kutengeneza mchanganuo wa kibiashara na kutoa udhamini
wa mkopo.
Aidha mkurufenzi huyo amesema kuwa Asasi hiyo ya kusaidia sekta binafsi ya
kilimo ipo tayari kumsaidia mtu binafsi,vikundi au makampuni kutumia huduma ya (Pass)haswa wajasiariamali binafsi amabao wana dira ambao wanafanya biashara katika hali ya ufanisi na
kibiashara.
kilimo ipo tayari kumsaidia mtu binafsi,vikundi au makampuni kutumia huduma ya (Pass)haswa wajasiariamali binafsi amabao wana dira ambao wanafanya biashara katika hali ya ufanisi na
kibiashara.
Sambamba
na hayo amesema ya kwamba asasi hiyo inashirikiana na benki washirika
zaidi ya 11 kupata mkopo kwa wakulima ambao wanaoweza kufikia angalau
vigezo vya msingi kwaajili ya ukopaji,huku kipaumbele kikitolewa kwa
wateja wenye matokeo makubwa katika mwendelezo wa
mnyororo wa thamani kwa bidhaa za kilimo hususani katika mazao ya chakula ,biashara na mazao ya kusafirishwa nje ya nchi.
mnyororo wa thamani kwa bidhaa za kilimo hususani katika mazao ya chakula ,biashara na mazao ya kusafirishwa nje ya nchi.
Ameainisha
mikoa ambayo Pass ipo nchini Tanzania kuwa ni Mwanza
,Kigoma,Kilimanjaro,Morogoro,Mbeya, Dar-es- salaam na Mtwara,amesema
wanatumia ofisi hizi za kanda ili kuwafikia wakulima kwa karibu zaidi.
0 maoni:
Chapisha Maoni