Posted by Esta Malibiche on JAN 31,2017 IN MICHEZO
Wachezaji wa Azam FC waliokuwa majeruhi ni nahodha John Bocco
‘Adebayor’, Stephan Kingue waliopata majeraha ya misuli ya paja kwenye
mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya
Simba, ambao matajiri hao walishinda bao 1-0 lililofungwa na Bocco.
Wengine wanaouguza majeraha, ambao waliukosa mchezo huo ni
kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kipa Mwadini Ally (nyama za paja) na
beki Shomari Kapombe, ambaye ni mgonjwa lakini hivi sasa akiendelea
vema.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz
mara baada ya mazoezi ya jana, Mwankemwa alisema kuwa Bocco na Kingue
watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili tokea jana, huku Sure Boy
akitarajiwa kuanza rasmi mazoezi leo na Mwadini akipumzishwa kwa siku
tatu kuanzia jana.
“Bocco hali yake inaonekana kuimarika vizuri tokea alipopata
majeraha hayo ya kuchana msuli wa nyuma ya paja, Stephan (Kingue) kwa
upande wake naye amechana msuli wa mbele ya paja, hivyo wote watakaa nje
ya dimba kwa muda wa wiki mbili kutoka sasa (jana) na wataanza mazoezi
mepesi baada ya wiki moja,” alisema.
Daktari huyo bingwa mzoefu, alisema hali za wachezaji wengine
ziko vizuri kabisa kuendelea na mikikimikiki ya maandalizi kuelekea
mechi zijazo za ligi pamoja na michuano mingine.
BAADA ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC,
kuanza rasmi mazoezi jana jioni kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya
Ndanda, daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, amezungumzia hali za
kiafya za baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.
0 maoni:
Chapisha Maoni