Posted by Esta Malibiche on JAN 27,2017 IN NEWS
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr
Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akishiriki kupalilia zao la mtama Mtama katika ziara aliyoifanya
Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi
akishiriki kupanda Mihogo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr
Rehema Nchimbi (wapili kutoka kulia) akishiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo katika ziara
aliyoifanya Mkoani humo.
Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki
chakula cha mchana baada ya kukaribishwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Mwenge Singida katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.
Viongozi,
Watendaji na Watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida wametakiwa
kuhakikisha taarifa zote za mapato na matumizi zinawafikia wananchi wote katika
ngazi ya Kata na Kijiji ili waweze kuelewa hasa kiasi cha fedha zilizoingizwa
na Serikali katika Halmashauri na namna zinavyo tumika.
Agizo
hili limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika ziara yake
ya kuzitembelea Halmashauri zote za Mkoa huo kwa lengo la kujenga Uelewa wa
pamoja, utumishi wa pamoja, na kasi ya pamoja ili kufikia lengo pamoja kwa
maslai mapana ya Taifa.
Kwa
upande wa Wakuu wa Idara na Vitengo Dkt Nchimbi amewaagiza wawe na taarifa za
kila siku za watendaji na watumishi katika mnyororo wote wa kiutendaji na
kiuongozi na kuepuka kutegemea taarifa za makaratasi na ili kuimrisha utendaji
wa kuzingatia matokeo yanayo onekana.
Niaibu sana kwa Mganga Mkuu wa Wiwala (DM)
kushindwa kutoa takwimu pale unapo ulizwa swali nje ya ofisi yako juu ya idadi
ya watoto waliozaliwa ndani ya siku tatu katika wilaya yako au Afisa Elimu wa
Halamashari unashindwa kutoa jibu la ni Walimu wangapi katika Halmashauri yako
hawakuingia kazini kwa sabau za kiafya. Sinto penda hali hii iendelee
kujitokeza katika Mkoa wa Singida. Aliongeza Dkt Nchimbi.
Mh
Dkt Nchimbi pia amewataka Watumishi wa umma Mkoani Singida kuzinduka usingizini
na kuacha kufikiri kuwa bado wapo katika kipindi cha uchaguzi na kuendekeza
siasa badala ya kufanya kazi ya kuwatumikia wanchi kwa uaminifu na uadilifu kama
inavyo taka serikali ya hawamu ya tano ya Tanzania chini ya Rais Dkt John
Joseph Pombe Magufuli.
Sinto mvumilia mtumishi yeyote wa umma ndani
ya Mkoa wangu wa Singida atakae shindwa kwendana na kasi ya Serikali ya hawamu
hii ya Tano, sitaki kuendelea kusikia msamiati wa Chini ya Kiwango katika
Ujenzi na wale wote watakao husika na ujenzi wa chini ya kiwango watakamatwa na
kulazimika kulipa thamani ya fedha zote zilizotumika katika ujenzi huo, watumishi
wa Umma ni lazima watambue kuwa wafanyapo kazi waweke mbele maslai ya umma
kwanza yaana wananchi kwanza. Alisema Mh Dkt Nchimbi.
Katika
suala la usalama wa Chakula Mh Dkt Nchimbi amelitaja kuwa ni wajibu wa kila
mmoja hivyo ni lazima Viongozi, Watendaji, Watumishi wa Halmashauri na Wananchi
kwa Ujumla wawajibike kwa pamoja kuhakikisha kuna usalama wa chakula hasa kwa
kulima Mazao yanayo tumia maji kwa ufanisi kama vile Mihogo, Mtama naViazi
lishe.
Dkt
Nchimbi amesisitiza kuwa viongozi na watendaji wote walime mashamba yasio
pungua nusu heka ya kilimo cha mihogo,
viazi lishe, mtama, Watumishi wa halmashauri zote wawe na mizinga isiyo pungua
miwili ya ufugaji nyuki na kila shule iwe na heka moja au zaidi ya Mihogo,
viazi lishe au Mtama, pia ziwe na nusu heka au zaidi ya mazao hayo kwaajili ya
walimu.
Ili
kutatua changamoto ya upungufu wa makazi ya watumishi wa Umma katika Mkoa wa
Singida Mh Mkuu wa Mkoa Dkt Nchimbi ameziagiza
Halmashauri zote za mkoa huo kuwapatia watumishi hasa walimu viwanja vya
kujenga nyumba za makazi kwa utaratibu ambao ni rafiki na mishahara yao na
licha ya kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi pia utaratibu huo utasaida
ustaafu mwema kwa watumishi wa Halmashauri hizo.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi amezindua shughuli mbali mbali za kilimo zenye kuzingatia mazao
yanayo tumia maji kwa ufanisi kama vile Mihogo, Mtama naViazi lishe na pia
amezindua Huduma maalum ya Afya katika Halamashuri ya Mkoa huo
0 maoni:
Chapisha Maoni