Posted by Esta Malibiche on JAN 3,2017 in SIASA
Katibu wa CCM mkoani Pwani,Hassan Mtenga akizungumza jambo katika kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Misugusugu.
Diwani wa viti maalum,Kibaha Mjini Selina Wilson akimwombea kura mgombea mteule kupitia CCM kata ya Misugusugu katika uzinduzi wa uchaguzi mdogo katika kata hiyo |
Mgombea mteule kupitia CCM kata ya Misugusugu,Ramadhani Bogas akiomba kura kwa wakazi wa Misugusugu katika uzinduzi wa kampeni
Baadhi
ya wana CCM na wakazi wa Misugusugu wakicheza katika uzinduzi wa
kampeni kata ya Misugusugu,uchaguzi katika kata hiyo unarejea baada ya
kutenguliwa na mahakama ya mkoa wa Pwani.
Katibu
wa CCM mkoa wa Kusini Unguja ,Sauda Mpambalioto ,akimuombea kura
mgombea mteule wa ugombea udiwani kupitia CCM ,Kata ya Misugusugu
Ramadhani Bogas.
Picha/stori Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
KATIBU
wa chama cha mapinduzi (CCM)mkoani Pwani,Hassan Mtenga,amevitaka vyama
pinzani viache kudanganya watanzania kuwa hakuna maendeleo yanayofanywa
na serikali na badala yake vifanye tathmini na kwenda na data ili kupata
majibu.
Aidha amesema mwenye macho aambiwi tazama
,ni ukweli unaoonekana kuwa serikali ya awamu ya tano kupitia CCM
inatekeleza ilani yake kwa kuleta maendeleo ya wananchi.
Akizungumza
katika uzinduzi wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya
Misugusugu ,Mtenga alisema wakazi wa kata hiyo wasikubali kudanganyika
wakati wanaiona serikali inavyochapa kazi.
Mtenga
alieleza kuwa ,wapinzani kwa sasa wamezimwa,hawana jipya ,wanatapatapa
hivyo watanzania wawapuuze kwa mambo ya uzushi wanayoyaibua.
Alisema
kuna kila sababu ya kuwajibu wachache wanaojaribu kuiharibia sifa
serikali kwa yale inayoyafanya ili kuwakomesha wasiendelee kuipaka
matope.
“WanaCCM
tafuteni kura kwa umoja wenu,msijiamini kwa kutafuta kura
majukwaani,kura hazipatikani kwenye majukwaa pekee ,fanyeni kazi,tumieni
maarifa ,piteni nyumba kwa nyumba kupata kuipa ushindi CCM”alisema
Mtenga.
Katibu
huyo wa CCM mkoani hapo,akijibu hoja zinazoibuliwa kwenye kampeni
zinazofanywa na Chadema katika kata hiyo, alieleza kwamba ,hali ya
kiuchumi wa Tanzania unaelekea kwenye asilimia 9 kutoka nne.
Aliwataka wasiropoke kwenye majukwaa pasipokuwa na tatwimu halisi,waache kuongea bila kuwa na data hali inayosababisha kupotosha watanzania.
Kuhusu
miundombinu alifafanua kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma ni km 641
ambapo watanzania wanatembea kwenye lami,Mtwara hadi Dar es salaam km
514,Dar es salaam-Iringa km 500.1 ni lami ,Dodoma –Mwanza km 334.Mwanza
-Geita kupitia Nyakanazi yenye km 644 nayo ni lami.
Mtenga
alisema Tanzania lazima ijivunie kuwa na miundombinu ya barabara bora
kwa kiwango cha lami ambapo kwasasa inafikia km 18,900.
Nae
katibu wa CCM mkoa wa Kusini Unguja ,Sauda Mpambalioto ,alimuombea kura
mgombea mteule wa ugombea udiwani kupitia CCM ,Ramadhani Bogas na
kusema anafaa kuwa kiongozi na sio bora kiongozi.
Alisema
upinzani haumaanishi hata penye sifa kukatolewa dosari na badala yake
kwenye sifa ama maendeleo haina budi pakaungwa mkono.
Sauda alisema CCM imefanya mengi ndani ya nchi tofauti na miaka 50 iliyopita hivyo ambae haoni maendeleo hayo ana lake jambo.
Mjumbe
wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kibaha Mjini, Rugemalira Rutatina,
aliwaasa vijana kuacha kutumika kama ngazi na watu wachache kwa maslahi
yao binafsi.
Rutatina
,alisema sio wakati wa kuchanganya madalanzi na machungwa hivyo wakazi
hao wachague diwani wa CCM ili kupiga hatua kimaendeleo.
Kwa upande wake ,mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala alisema anaimani na Bogas kwani ni mtu makini na muwajibikaji.
Aliwaomba wakazi wa Misugusugu kumchagua Bogas ili kutimiza majifya matatu ikiwa ni pamoja na rais,mbunge na diwani.
Mgombea udiwani kupitia CCM katika kata
hiyo,Bogas aliwaomba wakazi wa kata hiyo kumpa kura ili kushirikiana
kuinua maendeleo yao.
Aliahidi kutatua kero mbalimbali zinazogusa sekta ya elimu,afya,miundombinu kwa kuzifikisha sehemu husika na kupatiwa ufumbuzi.
0 maoni:
Chapisha Maoni