Posted by Esta Malibiche on JAN 19,2017 IN NEWS
Wenyeviti wa kamati za kudumu za halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakipitia kwa umakini makablasha ya bajeti.
Mkuu wa idara ya Fedha wa halmshauri Mr. Mhando akijibu maswali ya madiwani wakati wa kupitia bajeti ya kila idara na vitengo vya halmshauri ya Wilaya ya Mufindi.
Na Afisa Habari Mufindi
Baraza maalum la madiwani
wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, limejadili na kupitisha mapendekezo ya
bajeti ya halmshauri hiyo, yenye jumla ya Sh. bilioni 60.7 kwa mwaka wa fedha
wa 2017- 2018 huku kiasi kikubwa cha fedha hiyo ikikielekezwa kwenye miradi ya
maendeleo.
Taarifa
iliyotolewa na
kitengo cha habari na mawasilino cha halmshauri ya Wilaya ya Mufindi,
imebainisha sehemu kuu mbili za bajeti hiyo, ambapo jumla ya shilingi
bilioni
4.9 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida, bilioni 41.2 zikibajetiwa kwa
ajili ya mishahara ya watumishi wake, wakati bilioni 14.5 zikielekezwa
kwenye
miradi ya maendeleo.
Taarifa hiyo imevitaja
vyanzo vya mapato hayo, kuwa ni makusanyo ya halmashauri, fedha kutoka serikali
kuu, wafadhili, taasisi za kijamii sanjari na nguvu za wananchi.
Akizungumza wakati wa kuhailisha
kikao hicho, mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina amemtaka
Mkurugenzi mtendaji pamoja na wataalamu wake kuhakikisha wanaisimamia na
kuitetea bajeti kwa hoja zenye mashiko katika ngazi ya Mkoa na Taifa ili malengo ya kuharakisha maendeleo ya halmashauri yafikiwe kwa wakati na akawahimiza
watumishi na madiwani kushirikiana katika ukusanyaji wa mapato.
Kupitishwa kwa bajeti ya
na baraza la madiwani, ni kwa mujibu wa sheria ya fedha yaserikali za mitaa
namba 9 ya mwaka 2013. Aidha bajeti hiyo imezingatia mwangozo wa kitaifa wa
bajeti wa 2017/ 2018, ilani ya uchaguzi ya chama tawala CCM ya 2015/2020,
mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/2018 huku mambo mengine yakiwa ni
malengo ya maendeleo endelevu, dira ya Taifa ya maendeleo 2025 pamaja na
maelekezo ya kisekta na mpango wa
maendeleo ya miaka mitano.
0 maoni:
Chapisha Maoni