Posted by Esta Malibiche on JAN 19,2017 IN NEWS
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kushoto)
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza( kulia) mara baada
ya kuwasili mkoani huo kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya
Umeme Vijijini katika Mkoa huo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kulia) akisamilia na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC),
Livingstone Lusinde( kulia) walipowalisi mkoani wa Iringa, kwa ziara ya
kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini mkoani huo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kushoto) na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),
Livingstone Lusinde( kulia) wasikiliza hoja za Wajumbe wa Kamati ya PAC,
(hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi
ya Umeme Vijijini mkoani Iringa.
Wajumbe
wa Kamati ya PAC, wakisikiliza taarifa ya Mkoa wa Iringa, kabla ya
kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa MIRADI ya Umeme vijijini mkoani
Iringa.
Wajumbe wa Kamati ya PAC,wakikagua Miradi ya Umeme Vijijini katika kijiji cha Nyamahana mkoani Iringa.
Mjumbe
wa Kamati ya PAC, Shally Raymond( kulia) akisisitiza jambo kwa
wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua
utelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.
Mwenyekiti
wa Kamati ya PAC, Livingstone Lusinde ( kushoto) akiruka pamoja na
wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua Miradi
ya Umeme Vijijini.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kulia) akisalimiana
na wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua
Miradi ya Umeme Vijijini.
………………………..
Na Zuena Msuya, Iringa
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na
utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, Unaotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) katika Awamu ya kwanza na ya Pili ili kuona
thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika mradi huo.
Mwenyekiti
wa PAC, Livingstone Lusinde alisema hayo mkoani Iringa wakati wa ziara
ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA, katika vijiji na Taasisi
mbalimbali zilizopitiwa na Mradi huo.
Lusinde
alifafanua kuwa wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo baada ya
kuona miundombinu iliyotumika na maendeleo ya wananchi katika maeneo
ambayo yamepitiwa na miradi hiyo.
”
Tumepita katika vijiji mbalimbali hapa Iringa ambayo nimepitiwa na
REA,tumeona namna ambavyo mradi huo umetekelezwa na tumeona miundombinu
iliyotumika na maendeleo yake hivyo hatuna budi kusema wazi kuwa
tumeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu”, Alisema Lusinde.
Lusinde
aliwasisitiza wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Umeme vijijini,
kutumia miundombinu imara inayokwenda sambamba na thamani halisi ya
matumizi ya fedha za Serikali katika kutekeleza wa miradi hiyo ili
kutimiza malengo yaliokusudiwa na kuondoa hasara za makusudi zinazoweza
kujitokeza.
Vilevile
aliwataka wakandarasi hao kukamilisha zoezi za kuwaunganisha na huduma
ya umeme wananchi na Taasisi zilizoomba huduma hiyo katika maeneo
machache yaliyosalia ili kila mwananchi aliyeomba huduma hiyo aweze
kuipata kwa wakati na kuitumia.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini DKt. Medard Kalemani
alisema kuwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Vijijini
utashirikisha Viongozi Serikali za mitaa, Madiwani,Wabunge, Wakuu wa
Wilaya na Wakuu wa Mikoa.
Alifafanua
kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutoa fursa kwa wananchi kutoa
vipaumbele vya maeneo wanayotaka kufikiwa kwa huduma ya umeme kwa wakati
na kuvifikia vijiji vyote nchini.
”
Mradi wa REA Awamu ya Tatu utakuwa shirikishi, kwakuwa kabla ya
mkandarasi kuanza kazi yake, atatakiwa kuwasiliana na Viongozi wa
Serikali ya mitaa, Madiwani, Wabunge , Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa
ili wao watoe vipaumbe cha maeneo wanayotaka kufikiwa na mradi huo”,
alifafanua Dkt. Kalema.
Dkt.
Kalemani alibainisha kuwa utaratibu huo utawezesha kuviunganisha vijiji
vyote nchini na huduma ya umeme ili kutimiza azma ya Serikali ya
kufikia ya uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.
Kamati
ya Kudumu ya Hesabu za Serikali ( PAC) inafanya ziara ya kukagua Miradi
ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)kwa
kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini ( Tanesco) kwa lengo la kuona
thamani hali matumizi ya fedha ya Serikali katika mradi huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni