Posted by Esta Malibiche on JAN 19,2017 IN NEWS
Na Afisa Habari Mufindi
Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi imeendelea kustawi katika sekta ya elimu ambapo tathimini ya matokeo ya darasa la saba yanaonesha kupanda kutoka asilimia 80.39 mwaka
2015 hadi asilimia 84.90% mapema mwaka jana, ikiwa ni
sawa na ongezeko la asilimia 4.51 ikipishana kwa asilimia 03 pekee na mshindi wa
kwanza ambaye ni Manispaa ya Iringa mwenye asilimia 87.43.
Taarifa
ya Kitengo cha habari na mawasilino cha halmashauri, imetaarifu kuwa, hayo
yamebainishwa na ofisa elimu taaluma Bi. MARIAMU NGARA wakati wa kikao cha kila
mwaka cha thimini ya elimu ambacho huwakutanisha wakuu wa shule zote za msingi
na maaofisa elimu kata, ambapo tathimini ya ufaulu huo umejumuisha shule 143,
watahiniwa elfu 05 mianne 38 wavulana wakiwa elfu 02 miatatu 84 na wasichana ni elfu 03 na
54 huku wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya
Sekondari wakiwa ni elfu 4 miasita 17
sawa na asilimia 84.9.
Akisoma
taarifa hiyo Bi. NGALA ameainisha masomo ambayo wanafunzi wamefanya vizuri
zaidi kuwa ni pamoja na somo la Kiswahili ambalo ufaulu wake
ni asilimia 90. 51, Sayansi
90.13, Maarifa 87.88, Hisabati 56.34 huku somo la Kingereza likishika nafasi ya
ano kwa asilimia 27.20
Aidha,
afisa elimu huyo mwenye dhamana ya taaluma katika Wilaya, ametaja baadhi ya
malengo ambayo walijiwekea na ndiyo yaliyochangia kufikia mafanikio hayo kuwa
ni pamoja na kufaulisha kwa asilimia 95, ufuatiliaji wa utendaji kazi, uwepo wa
kambi za masomo, udhibiti wa utoro wa Wanafunzi na Waalimu, ukamilishaji wa
mada kwa wakati na uwepo wa mazoezi ya kujipima.
Idara
ya elimu msingi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imeweka uratibu wa kufanya
tathimini ya kina kwa kila mwaka mara baada ya kutoka kwa matokeo ya mitihani
ya darasa la saba ili kuangazia mafanikio ya ufaulu kwa kila shule, kubainisha
changamoto na kuziwekea mikakati ya kuzikabili huku tathimini hiyo ikienda
sanjari na kutunuku zawadi na vyeti kwa
wakuu wa shule na maofisa ilimu kata walifaulisha wanafunzi wengi zaidi hivyo
kupandisha wasitani wa ufaulu wa halmashauri.
0 maoni:
Chapisha Maoni