Posted byEsta Malibiche on JAN 13,2017 in NEWS
|
Mkuu wa
Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka waandishi wa habari kujiunga katika
vikundi vya ujasiliamaliili waweze kujiinua kichumi kupotia fursa zitolewazo na
taasisi za fedha na mifumo mbalimbali ya umma.
Kasesela alitoa kauli hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mashine ya kuoshea magari kwa kikundi cha ujasiliamali
cha waandishi wa habari mjini Iringa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Kasesela
alisema waaandishi wamekuwa wakitumiwa na watu wengi ususani viongozi kufukia
malengo yao lakini wamekuwa hawana msaada kwao mara baada ya
kufanikiwa.
“Mimi nitumie fursa hii kuwashauri
waandishi wa habari,ninyi ni nguzo muhimu katika nchi yetu,ni kioo cha jamii nammekuwa
chanzo cha mafanikio kwa watu wengi hususani viongozi, lakini niseme tu
nimekuwa nikisitishwa na pale watu wanapofanikiwa hushindwa kurudi kuwabeba ninyi”alisema
Kasesela.
Kasesela aliwataka viongozi na makundi
ya watu wengine kuhakikisha wanatoa
ushirikiano kwa waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kusaidia vikundi vyao
vya ujasimalia ili
waweze kunufaika na mafanikio
yaliyofikiwa.
>Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya alishauriwaandishi na makundi
mengine wanapoanza mwaka huu wa 2017 wajenge utamaduni wa kujituma katika kufanya
kazi na kuwa na
shughuli za ziada ili kujiongezea
kipato.
“Tupambane na umasikini,mwaka wa 2016
umeisha yatupasasasa kujitafakari,wapo tulikosea na wapo tumefanikiwa lakini
jambo la msingi katika kipindi cha mwaka 2017 nito wito kwenue waandishi na
kwa makundi mengine kufanya kazi kwa bidii na kuwa na shughuli
za ziada zenye
kuwaongezea kipato”alisema Kasesela.
Awali mwenyekiti wa kikundi hicho Frenk
Leonard alimshukuru Mkuu huyo wa Wilaya na kufafanua kuwa mashine hiyo pamoja na
mchango wa ununuzi w atangi wa Sh 100,000 aliotoa vitatumika
kwa mafufaa ya wanakindi.
“Nitumie fursa hii kukushuru wewe kwa moyo wako wa ukarimu,kama miezi miwili iliyopita
tulikuja a wazo letunawe hukusita akatutaka tuje na mchanganuo ,tumekuletea na
leo umetekeleza,nisema tunakushuru sana na nikuhakikishe mashine hii tutaitumia
kwa uadilifu na kwa malengo
yaliyokusudiwa”alisema Leonard.
Kwa upande
wake Tukuswiga Mwaisumbe ambaye ni mwanachama wa kikundi hicho alisema msaada
huo umejenga morali kwawanakikundi wa kuendelea kujitafutia kipato badala
ya kutegemea mshahara pekee ambao hautoshi kukidhi mahitaji yakila siku.
|
|
|
0 maoni:
Chapisha Maoni