Posted by sta Malibiche on JAN 23,2017 in Michezo
Na Emanuel Masaka, Globu ya Jamii
LIGI
ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga (Ulega Cup) imefunguliwa rasmi jana
kwa kuzikutanisha timu za Kipalang'anda kombaini Fc na Mkuranga
kombaini uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
Mashindano hayo yamefunguliwa na mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto
Sanga ukishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega, Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed pamoja na baadhi ya
madiwani wanaounda halmashauri hiyo.
Michuano
hiyo ambayo ilianzia ngazi ya Vijiji ilishirikisha timu 125 na baadae
kuchujwa na kubakia timu 25 ambazo zimeingia ngazi ya wilaya na mshindi
wa ligi hiyo ndio atakuwa bingwa wa wilaya.
Akizungumza
na wachezaji wa timu hizo katika ufunguzi wa michuano hiyo Mkuu wa
Wilaya hiyo Firbato Sanga alisema michezo ni udugu na ujirani mwema
hivyo aliwatakia michezo mwema.
Akizungumzia
michuano hiyo Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega amesema kuwa ni
matarajio yake michuano hiyo itakwenda vyema na lengo lake kubwa
nikuona wanapata vijana wenye vipaji na watakaoweza kuipaisha Mkuranga.
"Nimatarajio
yangu mambo yatakwenda kama nilivyopanga na kama mnavyoona wenyewe
waandishi wa habari vijana wa kutoka Mkuranga ndio wanaocheza "alisema
Ulega
Amesema
tangu awali alisha kataa timu hizo kukodi watu Kutoka nje ya Mkuranga
na anashukuru Mungu hayo yamezingatiwa na katika michuano hiyo mshindi
ndio atakuwa bingwa wa Wilaya.
Amesema
kuwa ana matumaini makubwa kwamba kupitia ligi hiyo watapatikanika
vijana wenye uwezo ambao wataweza kuchukuliwa na timu kubwa.
Aidha
amesema kuwa michezo ni Afya ,ajira,na upendo kwani kupitia mashindano
hayo watakuwa wametengeneza ujirani mwema hivyo watumie fursa hiyo
kudumisha Umoja na mshikamono miongoni mwao.
Mchezo
huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na mchezaji wa timu ya
Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed katika dakika ya kumi kipindi cha
kwanza.
Mbunge
wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga
(Ulega Cup) uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga
mkoani Pwani
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga
akizungumza na wachezaji wa timu za Kipalang'anda kombaini Fc na
Mkuranga kombaini katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga
(Ulega Cup) uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga
mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga
akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma
Abed katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga
akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini
pamoja viongozi mblimbali katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga
mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga
akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kipalang'anda
kombaini Fc katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
.Sehemu ya mashabi wa timu ya Kipalang'anda kombaini Fc na Mkuranga kombaini wakiwa wakishuhudia mtanange katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani
.Mchezo
ukiendelea ambapo mchezo huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na
mchezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed katika dakika
ya kumi kipindi cha kwanza.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Pwani.
0 maoni:
Chapisha Maoni