Jumanne, 3 Januari 2017

MWANSASU AANZA KUPATA MATUMAINI YA BEACH SOCER



Posted by Esta Malibiche on JAN 3,2017 in MICHEZO


mwansasu-mbeya
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya mpira wa ufukweni,maarufu kama Beach Socer,John Mwansasu amesema kwamba baada ya wadhamini kuanza kujitokeza kudhamini mchezo huo,anaamini Tanzania itafanya vizuri kwenye michuano mbalimbali.
Mwansasu ameyasema hayo baada ya kampuni ya simu ya TTCL kujitokeza kudhamini bonanza la mashindano ya beach soccer kwa vyuo vikuu vya Dar es salaam yatakayoanza kufanyika siku ya tarehe saba katika viwanja vya coco beach.
Amesema kwamba timu ya Taifa ya beach soka inaundwa Zaidi na wanafunzi wa vyuo,hivyo kwa kuanzishwa kwa bonanza hilo ambalo litahusisha vyuo mbalimbali kwake kutampa wigo mpana wa kupata wachezaji ambao watakuwa msada kwa timu ya Taifa.

0 maoni:

Chapisha Maoni