Ijumaa, 13 Januari 2017

TAIFA ‘STARS’ YAPEWA KUNDI RAHISI KUFUZU AFCON 2019

Posted by Esta Malibiche on JAN 2017 In MICHEZO

Taifa-Stars-of-Tanzania- TANZANIA
Baada ya kusota kwa miaka kadhaa timu ya taifa ya Tanzania ‘Stars’kupangwa kwenye makundi magumu hatimaye CAF imeipa ahueni na kuipanga katika kundi L, kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon pamoja na Uganda, Cape Verde na Lesotho. Hili linaweza kuwa kundi rahisi zaidi Taifa Stars, kwani zote Uganda, Cape Verde na Lesotho ni timu ambazo zipo ndani ya uwezo wake – kikubwa ni maandalizi ni mshikamano wa Watanzania kama taifa. Kenya pia itaanzia hatua ya makundi, ikiwa imepangwa Kundi F pamoja na Ghana, Ethiopia na Serra Leone, wakati Rwanda ipo Kundi H pamoja na Ivory Coast, Guinea na Afrika ya Kati (CAR).
Mshindi wa kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON ya 2019, wakati timu nyingine tatu zitakazomaliza nafasi ya pili na wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama washindi wa pili bora. 
Michuano hiyo itaanzia kwa hatua ya mchujo, Raundi ya Awali itakayohusisha timu za Comoros, Djibouti, Madagascar, Mauritius, Sao Tome E Principe na Sudan Kusini.
Timu zitakazofuzu hapo zitaingia moja kwa moja kwenye makundi A, B na C kukamilisha idadi ya timu nne nne. Kundi Ab lina timu za Senegal, Equatorial Guinea na Sudan, B kuna wenyeji Cameroon, Morocco na Malawi na C kuna Mali, Gabon n Burundi.
Cameroon ikiongoza Kundi, mshindi wa pili atafuzu moja kwa moja na kama itashika nafasi ya tatu au ya nne, mshindi wa kwanza atafuzu moja kwa moja na mshindi wa pili atawania nafasi tatu za ziada za kufuzu kama mmoja wa washindi wa pili bora. 
Hatua ya mchu itachezwa kati ya Machi 20 na 28 wakati mechi za kwanza za makundi zitaanza Juni 5 na 13, za pili Machi 19 na 27 2018, za tatu Septemba 3 na 11, 2018 za nne Oktoba 8 na 16, 2018 na za tano Novemba 5 na 13, 2018.
 
 
 
 

0 maoni:

Chapisha Maoni