Posted by EstaMalibiche on JAN 5,2017 in NEWS
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiagana na watoto wa kike walio katika mpango wa kuwezeshwa kijasiriamali na Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) |
Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga
akiongea na wazee wa kimila kutoka koo tano mkoani Mara ambapo
amewapongeza kwa kazi ya kuelimisha jamii inayowazunguka juu ya madhara
ya ukeketaji kwa watoto wa kike na tohara mara mbili kwa watoto wakiume,
Katikati ni Mtumishi Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) Bi. Kambibi Kamugisha,
kushoto ni Katibu Tawala Tarime Bw. John Marwa na Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai.
Mzee wa Kimila kutoka Koo ya
Bukira Mzee Sinda Nyangore akiongea na na Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo
alishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote
vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji
kwenye koo mbalimbali.
Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias
Maganya akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alimuomba Katibu
Mkuu kuangalia uwezekano wa kuwezeshwa kutembea Koo hadi Koo kwa ajili
ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.
Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa
katika picha ya pamoja na wazee wa kimila kutoka koo tano za
Bukenye,Nyabasi,Bukira,Butimbaru na Buhunyaga leo Mjini Tarime
Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga
akiongea na watoto wa kike walio katika mradi unaotekelezwa na Jukwaa la
Utu wa Mtoto(CDF) wa kuwawezesha kijasiriamali watoto waliokimbia
vitendo vya ukeketaji.
Katibu Mkuu Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) na
watoto wakike walio katika mradi huo.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wazee wa Kimila kutoka Koo Tano
Mkoani Mara wamemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuwawezesha kutembea Koo
hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.
Akiongea wakati walipokutana na
Katibu Mkuu aliyepo Wilayani Tarime Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias
Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda
Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine
Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.
“Tumechoka vitendo vya ukatili kwa
watoto na vitendo visivyoturishisha sisi kama wazee, tutafanya kila
jitihada kuweza kuondokana na vitendo hivi, tunahitaji ushiriki zaidi wa
serikali na asasi nyingine zishirikiane na CDF ili kwa pamoja tuweze
kufikia lengo tuliloliweka” Alisema Mzee Elias
Akitolea ufafanuzi suala hilo
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga amesema kweli upo umuhimu wa kutekeleza suala hilo la
kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili kuweza kuwasaidia watoto
wakike.
Naye Mzee wa Kimila kutoka Koo ya
Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri serikali na mashirika mengine
kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa
elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.
Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu
Sihaba Nkinga alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia
katika wilaya hiyo na kujionea namna wanavyofanya kazi na jinsi
wanavyokabiliana na changamoto mablimbali.
Aidha Bi. Sihaba aliwatembelea
watoto wa kike waliopo katika mpango wa uendelezwaji kijasiriamali
unaotekelezwa na Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) katika kata ya
Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara.
0 maoni:
Chapisha Maoni