Jumamosi, 14 Januari 2017

DC IKUNGI MIRAJI MTATURU AAGIZA KILA KAYA KUPANDA MITI 10 KWA MWAKA.

Posted by Esta Malibiche on JAN 14,2017 IN NEWS

IKUNGI 2
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akipanda mti katika shule ya sekondari Unyihati iliyopo wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa  wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.

 IKUNGI 1
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akishirikiana na Kaimu Afisa misitu wa Wilaya hiyo Bosco Ndunguru kuweka udongo kwenye mti alioupanda katika shule ya sekondari Unyihati wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.
 IKUNGI 2
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akipanda mti katika shule ya sekondari Unyihati wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.


IKUNGI
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akimwagilia maji kwenye mti alioupanda katika shule ya sekondari Unyihati iliyopo wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa  wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.

 IKUNGI 3
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Miraji Mtaturu akizungumza na watendaji wa Wilaya hiyo na wananchi baada ya kuzindua upandaji miti.
…………….

MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu ameziagiza kaya zote zilizopo katika wilaya hiyo kupanda miti 10 kwa mwaka na kuitunza ili kukabiliana na ongezeko la joto la dunia.
Agizo hilo linahusisha  pia vijiji na taasisi zilizopo wilayani humo.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika katika shule ya sekondari ya  Unyahati mkuu wa wilaya huyo alisema lengo la wilaya ni kupanda miti 550,000 kwa mwaka.
“Naelekeza kila tarafa kuwa na kitalu cha miche ya miti ili iwe rahisi wananchi kupata miche na kutimiza lengo tulilojiwekea”,amesema Mtaturu.
Mbali na hilo ameitaka  halmashauri kuweka sheria ndogo ili kusaidia utekelezaji wa mipango ya idara ya misitu waliyojiwekea.
Ametaja changamoto iliyopo katika utunzaji wa mazingira kuwa ni ufugaji holela na ukame na kuwataka wananchi kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.
Mtaturu amewapongeza wadau wa mazingira kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika utunzaji wa mazingira.

Kauli mbiu ya uzinduzi huo ni panda miti ikutunze ambapo katika uzinduzi  wamefanikiwa kupanda miti ipatayo 2500.

0 maoni:

Chapisha Maoni