Posted by Esta Malibiche on JAN 23,2017 IN NEWS
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Eng. Stella Manyanya
akisalimiana na wanafunzi wa shule za msingi za Mwaya na Tumaini
zilizopo kata ya Nyalumbu wilayani Kilolo, mkoani Iringa wakati ya ziara
ya ufuatilialiaji wa vituo vya elimu nje ya mfumo rasmi, vituo sitiri
na elimu ya watu wazima juzi.
NAIBU
wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Eng. Stella Manyanya
amesikitishwa na kiwango cha hali ya kutojua kusoma, kuandika na
kuhesabu (illiteracy rate) katika Mkoa wa Iringa, ambayo ni asilimia 18.
Mkoa wa Iringa una jumla ya watu 941,238 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Eng.
Manyanya aliyasema hayo juzi wakati ya ziara yake ya ufuatilialiaji wa
vituo vya elimu nje ya mfumo rasmi, vituo sitiri na elimu ya watu
wazima, mkoani Iringa.
Alisema
kuwa takwimu hizo za kuongezeka watu wasiojua kusoma, kuandika na
kuhesabu zinahitaji juhudi za serikali ili kufikia malengo ya kimataifa.
Alisema
kuwa anatamani kuona katika sensa ya watu na makazi inayokuja fungu la
watu wasiojua kusoma na kuandika mkoani Iringa na kwa nchi nzima
linapungua.
Wakati
wa ziara hiyo eng. Manyanya litembelea shule za msingi za mwaya,
tumaini, ikuvala, mtua, kilalakidewa na ibumu zote za wilaya ya kilolo,
mkoani Iringa.
Akiongea
na wananchi wa kijiji cha kilalakidewa kata ya ibumu kitongoji cha
vigulu, katika mkutano wa hadhara, naibu waziri wa elimu aliwataka
wazazi na walezi kuhakikisha wanaandikisha watoto wote wenye umri wa
kwenda shule ili kupunguza tatizo la watu wasiojua kusoma na kuandika.
Awali,
mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla akitoa taarifa ya wilaya yake kwa
naibu waziri wa elimu, alisema kuwa wilaya ina jumla ya watu wazima
10,373 wakiwemo wanaume 3,892 na wanawake 6,482 ambao hawajui kusoma,
kuandika na kuhesabu.
Alisema kuwa taarifa hiyo ni kwa mujibu wa takimwu zilizokusanywa na idara ya elimu katika kipindi cha mwaka 2016 mwezi Oktoba.
Mkuu
wa wilaya huyo alisema kuwa atahakikisha wilaya yake inatekeleza jukumu
la kutoa elimu kwa watu wote na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri
wa kwenda shule anapata fursa ya elimu.
Wilaya
ya kilolo ina jumla ya vituo tisa (9)vya mpango wa elimu ya msingi kwa
walioikosa (MEMKWA) vyenye jumla ya wanafuzi 198 kati yao wavulana 121
na wasichana 77.
Kwa
upande wake, kaimu afisa elimu wa mkoa wa iringa, Richard Mfugale kwa
niaba ya katibu tawala wa mkoa, asilimia kuwa mkoa wa unaendesha program
za elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.
Alisema kuwa mkoa una jumla ya vituo vya MEMKWA 18 vyenye jumla ya wafunzi 338 kati ya hao wavulana 205 na wasichana ni 133.
Mfugale alisema kuwa utoaji wa elimu ya watu wazima unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wake.
Alizitaja
baadhi ya changamoto hizo kuwa ni honoraria kwa wawezeshaji wa program
na kusababisha wawezeshaji kuacha na kutafuta shughuli zingine.
Changamoto
zingine ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na
uhaba wa rasilimali fedha kwa ajili ya ufuatiliaji wa program hiyo ya
MEMKWA.
Alisema
kuwa changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti ya ufuatiliaji wa program
hiyo katika kitengo cha elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo
rasmi.
Wakati
huohuo, naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Eng. Stella
Manyanya amesikitishwa na hali ya miundombinu ya madarasa ya wanafunzi
wa MEMKWA katika baadhi ya shule za msingi wilayani Kilolo, mkoani
Iringa isiyoridhisha.
Aidha,
Eng. Manyanya alitoa rai kwa wakuu wa shule nchini wanatakiwa kuwa na
madarasa ya MEMKWA katika shule zao na kuagiza kuachana na walimu wa
kujitolea wanaofundisha madarasa hayo.
Alisema
kuwa baadhi ya shule zina walimu wakutosha hivyo watumie rasilimali
watu zilizopo kufundisha madarasa ya MEMKWA ili kupunguza ubaguzi kwa
wanafunzi wa MEMKWA kwa kuwaita wanafunzi wa elimu nje ya mfumo rasmi,
bali waitwe wanafunzi.
0 maoni:
Chapisha Maoni