Posted by Esta Malibiche on JAN 16,2017 in NEWS
Mbunge wa jimbo la Chalinze [CCM]Ridhiwani Kikwete akipokea Madawati toka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Singh.Aliyesimama katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiwangwa Ndg. Rashid
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa tatu kutoka kushoto,akiwa na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Singh Bwana Kugis wa pili kutoka kulia,pamoja
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo wa kwanza kushoto baada ya kupokea msaada wa
madawati kutoka Jumuiya hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze akipanda mti kuashiria sherehe ya miaka 350 toka kuzaliwa kwa Guru Sing Sikh.
Jumuiya
ya Singh maarufu kama masingasinga hapa nchini imetoa msaada wa
madawati 100 na meza 100 ,vyenye gharama ya mil. 5,kwa shule ya
sekondari ya kata ya Kiwangwa,chalinze wilaya ya Bagamoyo.
Jumuiya hiyo imetoa msaada huo ,ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu.
Akiongea
kwa niaba ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Kurgis,katibu wa Jumuiya hiyo
ya Singh bw .Singh alisema ubora wa upatikanaji wa elimu katika shule
unategemea mchango wa kila mdau hivyo wao wameamua kuanza na madawati .
Alisema lengo ni kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri na hatimae kutimiza ndoto zao.
,"Ndugu
zangu sisi Singasinga tumeamua kuanza na madawati lengo letu ni kuona
watoto wakisoma katika mazingira rafiki,hatimae waweze kufika mbali
kielimu”alisema Kurgis .
Akizungumza
katika hafla ya upokeaji wa madawati hayo mgeni rasmi, mbunge wa
Chalinze, Ridhiwani Kikwete,aliishukuru jumuiya ya Singasinga kwa msaada
huo na kusema utasaidia watoto kuondokana na adha ya kukaa chini .
"
Leo tunawashukuru kwa madawati lakini tatizo la maji na umbali wa
wanapoenda kuchukua maji vijana wetu unasababisha pia kushuka kwa
viwango vya ufaulu sio tu shuleni hapa lakini katika maeneo mengi ndani
ya halmashauri yetu.alieleza Ridhiwani.
Ridhiwani aliwaomba wajaribu kusaidia changamoto hiyo kwa kuiweka kwenye mipango yao kazi ya maendeleo ya jamii.
Alifafanua
endapo jumuiya hiyo itasaidia kuchimba visima italeta tija katika
maeneo mengi jimboni hapo maana pia watoto wanateseka kutokana shule
nyingi hazina huduma ya maji.
Ridhiwani alisema kijumla Jimbo hilo limeshakamilisha kutatua tatizo la upungufu wa madawati na wanashukuru kupata ya ziada.
Mbunge
huyo alisema kwasasa nguvu zao zinaelekezwa katika ujenzi wa madarasa
mashuleni na kukarabati yale chakavu hivyo aliwaomba wadau wa maendeleo
wajitokeze kuunga mkono suala hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni