Jumatano, 18 Januari 2017

SIJASTAAFU KUFUNDISHA SOKA-LOUIS VAN GAAL

Posted by Esta Malibiche on JAN 18,2017 IN MICHEZO

Tottenham-Hotspur-FC-Courting-Louis-van-Gaal
Aliyekuwa meneja wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa hajastaafu na kwamba anachukua likizo ya mda.
Van Gaal mwenye umri wa miaka 65 hajajiunga na timu nyengine tangu aondoke Old Trafford mnamo mwezi Mei.
Siku ya Jumatatu, gazeti moja la Uholanzi De Telegraaf lilisema Van Gaal amemaliza muda wake wa ukufunzi na amestaafu kama mkufunzi ,hatua ilioshinikizwa na kifo cha mwanawe.
Lakini alikiambia kituo kimoja cha redio nchini Uhispania Cadena Ser kwamba ijapokuwa kustaafu kunawezekana bado hajaamua.
Raia huyo wa Uholanzi pia alifichua kwamba amekataa kuifunza klabu ya Uhispania Valencia mwezi uliopita.
”Iwapo nitaendelea au la pia itategemea na maombi nitakayopata,aliongezea.
Nimevifunza vilabu vingi na nadhani ni vigumu kuviinua vikiwa katika hali hiyo.
Sio kweli kwamba nimestaafu, sio sasa, lakini nitaamua mwisho wa likizo yangu mwezi Juni ama Julai”.

0 maoni:

Chapisha Maoni