Jumatatu, 30 Januari 2017

TAMASHA LA ARUSHA TOURISM FESTIVAL LAFANA ARUSHA, WATOTO WADOGO NAO WASHIRIKI NA MBIO

Posted by Esta Malibiche on JAN 30,2017 IN BURUDANI

Mgeni rasmi katika tamasha hilo Afisa michezo wa Jiji la
Arusha Benson Maneno akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa kwa upande
wa wanawake mbio za kilometa 3000 zawadi,ambapo mshindi wa kwanza
Anjeline Tsere alitumia dakika 9:39.96,Jacline Sakilo alitumia dakika
9:44.13,na wa tatu Secilia Ginoka ametumia dakika 9:45 .Picha na Vero
Ignatus Blog
Pichani ni Katibu wa chama cha
riadha mkoa wa Arusha Alfred Shahanga,ambaye pia ni muaandaaji wa
Arusha Tourism Festival Picha na Vero Ignatus Blog.

Pichani Mussa Juma ambaye ni  Mkurugenzi wa Arusha
Media  ambaye ni muandaaji wa Arusha Tourism Marathon
Festival.
Wa kwanza kushoto ni mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji
Arusha,Andrew Ngobole ambaye pia ni mmoja wa waandaaji wa mashindano
hayo kutoka Arusha media akisalimiana na katibu wa chama cha riadha
mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kikundi cha Ngoma kutoka jijini Arusha kijulikanancho kama Mtikisiko
sanaa group wakitoa burudani katika mashindano hayo ya Arusha Tourism
Marathon.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya wadau na washiriki katika mashindano katika
tamasha la Arusha Tourism Marathon wakiwa wanafuatailia yanayoendelea
uwanjani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog
Mshindi wa Arusha Tourism Marathon
Festival  akiwa anamalizia mbio za kilomita 5000 Emmanuel Giniki
ambate amepewa zawadi ya shilingi 200,000 pamoja na kupatiwa bonansi
ya kuongoza njia shilingi 50,000. Picha na Vero Ignatus
Blog
.
 
Mshindi wa pili wa mbio za kilometa 5000 za
Atusha Tourism Marathon  Gabriel Geay ametumia dakika
14:05:08.Picha na Vero Ignatus Blog
Wakwanza kutoka kulia ni mkurugenzi wa Arusha Media Musa Juma akimnyanyua mkono mshindi wa Arusha Tourism Marathon Emmanuel Giniki katikakatika mashindano hayo,Kutoka kulia ni Katibu wa chama cha Riadha mkoani Arusha Alfredy Shahanga ,akifuatiwa na mshindi wa tatu Ismail Juma ambaye alimaliza mbio hizo kwa kutumia dakika 14:11.60,akifuatiwa na mshindi wa pili Gabriel Geay  .Picha na Vero Ignatus Blog
Afisa michezo Jiji la Arusha Benson Maneno wakwanza
kushoto akijiandaa kuzindua mbio maalum za watoto wadogo walioshiriki
katika Arusha Tourism Marathon akiwa pamoja na mwenyekiti wa Marathon
mkoa wa Arusha
 
Watoto wakiandwaliwa tayari kwa kukimbia mbio za mita
hamsini leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid,na wao wameshiriki
katika Arusha Tourism Marathon.Picha na Vero Ignatus
Blog.
Wakwanza kulia namba 043ndiye mshindi wa kwanza kwa wanawake
katika mbio za kilometa 200
ambapo ametumia dakika 29:04,akifuatiwa na mshindi wa pili aliyepo
katikati Susan Patric kutoka Arusha miaka( 20)ambaye ametumia dakika
29:31 na mshindi wa tatu ni Neema Kasunda (20)ametumia dakika
29:89.Picha na Vero Ignatus Blog

Mtoto huyu naye ameshiriki mbio mita 50 katika tamasha la Arusha
Tourism Marathon .Picha na Vero Ignatus blog




Haji Mbuguni kutoka kutoka Chama cha waongoza Utalii Tanzania ,ambaye
anashughulika naIdara ya mazingira, uhusiano,na uhamasishaji ,yeye nae
ni mdau wa utalii na ameshiriki katika tamasha la Arusha Tourism
Marathon Festival (Utalii na michezo inawezekana)Picha na Vero Ignatus
Blog.



Na.Vero Ignatus ,Arusha

Tamasha la Arusha tourism marathon limefanyika Leo jijini Arusha
ikiwa ni awamu ya pili kufanyika mkoani haha ambapo mashindano hayo
yameandaliwa na Arusha Media, Shahanga sport promotion
Chini ya udhamini wa Tanapa.
Tamasha hilo
limewashirikisha wanariadha kutoka mkoa wa Arusha, Manyara,pamoja na
Kilimanjaro ambapo tamasha hilo likiwa limebeba kauli mbiu ya piga
vita ujangili, tembelea Hifadhi zetu.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Afisa michezo wajiji la Arusha
Benson Maneno ambapo amesema kuwa riadha imeutoa mkoa
wa Arusha kimasomaso na Tanzania kwa ujumla michezo mingine bado
imedorora
Amekipongeza chama cha riadha mkoa wa Arusha na
kuwataka kuongeza juhudi zaidi kwani michezo ni ajira,hujenga mwili
kiafaya ,pia michezo humtambulisha mtu kitaifa na kimataifa pia,
amewataka vijana kuchangamkia fursa hayo.
Katibu wa riadha
mkoa wa Arusha kuwa Alfred Shahanga ambapo pia ni muandaaji mwenza
wa Arusha Tourism Festival amesema kuwa mashindano hayo yalianza
mwaka 2015 walianza na mbio za barabarani huku safari hii wameamua
kurudi uwanjani ili kuhamasisha mbio fupifupi ambazo kuwamuda mrefu
zimesahaulika.
“Mashindano haya kwetu sisi yameonyesha
ufanisi mkubwa kwani mshindi wa kwanza katika mbio za mita 5000
ameweka rekodi ya uwanja namaanisha muda aliokimbia ni rekodi ya
uwanja huu.”alisema Shahanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Arusha Media Mussa Juma amesema kuwa lengo kubwa la mashindano hayo ni
kuhamasisha michezo katika mkoa wa Arusha pamoja na kuutangaza Utalii
wa ndani
“Tumewashirikisha watoto wadogo katika mashindano
haya kwani hawa nimabalozi wabaadae ambao watakuja kupiga vita
ujangili,watawahamasisha kizazi kijacho michezo , na watautangaza
vyema utalii wandani hapo badge.”alisema Mussa.

Mashindano hayo yameambatana na utoaji wa zawadi kwawashindi ambapo
wasindi wa mbio za kilometa 3000 kwaupande wanawake mshindi wa kwanza
alipewa zawadi ya shilingi 150,000 na wale wa mbio za kilomita 5000
mshindi wakwanza amepatiwa zawadi ya shilingi 200,000.

0 maoni:

Chapisha Maoni