Alhamisi, 19 Januari 2017

LAANA TUPU IRINGA KAKA AMBAKA DADAKE AMTOA USICHANA WAKE

Posted by Esta Malibiche on JAN 19,2017 

LAA
Afisa  maendeleo ya  jamii Manispaa   ya  Iringa  Josephina Mwaipopo  akiwa na mtoto aliyebakwa
DC
Richard  kasesela  akiwa amemnyanyua  mtoto  aliyebakwa  akitokanae
kuchukuliwa  vipimo Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa
 Watuhumiwa  baba  na mwanae  wakiwa   chini ya  ulinziNa MatukiodaimaBlog  YAWEZEKANA
ikawa  ni  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa kunyesha  mkoani Iringa
tofauti  na  ilivyozoeleka  miaka  mingine  ni  kutokana na laana kama
hizi  baada  ya kikosi  maaalum kinachoongozwa   mkuu  wa  wilaya ya
Iringa  Richard Kasesela  kwa  kushirikiana na OFM kufanikiwa
kumkamata  kijana Emmanuel Mkiwa  (19) kwa tuhuma  za kumbaka mara kwa
mara mdogo wake  wa miaka (4)

 
 
Imedaiwa
kuwa kijana  huyo  ambae  ni mwenyeji  wa mtaa  wa Omary  Matrekta kata
ya  Mtwivila  katika  Manispaa ya  Iringa alikuwa akiishi nyumba  moja
na babake pamoja na wadogo  zake watatu  wawili  wa  kiume na mmoja
ni  mtoto   huyo  wa  miaka 4  ambaye alitelekezwa  na mamake  mzazi
kutokana na mambo ya  kifamilia kati  yake baba  wa  mtoto .
 
Mashuhuda
wa  tukio   hilo  lililotokea January 16 majira ya  saa 2 usiku
walimweleza  mwandishi  wa  OFM  Iringa  kuwa kijana   huyo mara  kwa
mara  alikuwa  akimbaka  mdogo wake  huyo  ambae baba  mmoja  na mama
tofauti kabla  ya  mtoto   huyo kuwaeleza majirani   kuwa kakake  huyo
amekuwa akimkandamiza na  kijiti sehemu  zake  za  siri (Akimbaka)
 
Kutokana
na  maelezo ya  mtoto   huyo ndipo taarifa  za  raia  wema  hao
zilipofikishwa kwa mkuu  wa  wilaya  na OFM na  kuamua  kufika  katika
eneo la  tukio na  kufanikiwa  kumkamata kijana   huyo  na baba mzazi
wa  watoto  hao  Shukuru Mkiwa kwa malezi mabaya  ya  watoto.
 
Akizungumza
baada ya  kukamatwa  kwa  kijana   huyo  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa
Richard  Kasesela   pamoja na  kuwashukuru raia wema  kwa  kufikisha
taaarifa  ya  kunyanyaswa  kwa mtoto   huyo  bado  alitoa wito kwa
wananchi  wengine  ambao  wanataarifa  za  kunyanyaswa  kwa  mtoto
yeyote  katika  wilaya ya  Iringa  kutoa taarifa  ili  wahusika
wakamatwe  na  kufikishwa  katika  vyombo  vya sheria.
 
Kasesela
alisema  kuwa uchunguzi   uliofanywa baada ya  vipimo katika  Hospitali
ya  Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa umeonyesha mtoto   huyo kashaondolewa
usichana wake   na  hivyo kulazimika  kulazwa  kwa  matibabu
katika Hospitali   hiyo huku akiahidi kumsaidia mtoto  huyo  kumsomesha .
 
Alisema
kuwa yawezekana  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa  kunyesha katika
mkoa  wa Iringa  ni  pamoja  na matukio ya  kinyama kama haya ya
ubakaji  watoto na  kuwa  hatakubali kuona mbakaji  anaendelea   kuishi
uraiani wilaya ya  Iringa kwani tayari  mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa
Amina Masenza  kupitia  kikao  cha makati ya  ushauri ya  mkoa (RCC)
aliagiza wabakaji wote wasakwe kwa udi na uvumba na yeye ameanza
kutekeleza agizo hilo.
 
Japo
alisema alishangazwa  na hatua ya baba  mzazi wa  kijana  huyo
kumficha mbakaji ndani na  kudanganya  kuwa  hayupo wakati  kijana
wake  alikuwepo  ndani hivyo  mzazi  huyo  kukamatwa pamoja na kijana
wake yeye kwa  kosa la  kumchifa  mharifu  na kijana wake kwa kosa la
ubakaji .
 
“Hiki  ni  kikosi  kamili  ambacho kitaendelea  kuendesha  misako  mbali mbali kwa kushirikiana na oparesheni  Fichua Maovu (OFM) ya
Global Publishers hivyo kwa  yeyote  anayejua  wapi  mtoto anafanyiwa
vitendo  vya kikatili piga  simu hii mwandishi wa OFM Iringa 0754 026 299 tutakufikia ulipo na
kuchukua  hatua”
 
Jeshi
la  polisi  mkoa  wa Iringa  kupitia kwa  kamanda wa  polisi  mkoa
(RPC) Julius Mjengi limethibitisha  kukamatwa kwa mtuhumiwa   huyo na 
kuwa baada ya  upalelezi  atafikishwa mahakamani  huku  likiwataka 
wananchi  kuendelea  kufichua  waharifu  zaidi
 

0 maoni:

Chapisha Maoni