Posted by Esta Malibiche on JAN 26,2017 IN NEWS
Na Nathaniel Limu, Singida
Halmashauri ya Manispaa ya Singida
inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 13.1 bilioni, kwa ajili ya
kugharamia miradi mitatu ya uimarishaji miji (ULGSP) inayogharamia na
benki ya dunia.
Hayo yamesemwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Bravo Kizito Lyapembile, wakati
akizungumzia kwenye hafla ya sherehe ya kusaini mkataba baina ya
manispaa, washauri na mkandarasi atakayetekeleza miradi hiyo.
Alisema wamefikia hatua hiyo ya kusaini mkataba baada ya taratibu zote za kisheria za manunuzi kukamilika.
Alisema miradi hiyo ni ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 5.75 kwa kiwango cha lami.
“Barabara hizo ni pamoja na ile
inayoanzia kituo cha mafuta namfua hadi ofisi ya mamlaka ya mapato
(TRA), ambaye itapanuliwa na kuwa mbili (double road). Nyingine ni ile
inayoanzia ofisi za TRA hadi makazi ya Askofu wa Kanisa la Katoliki
(barabara ya Kinyeto),” alisema.
Mkurugenzi
Bravo Kizito Lyampembile (wa kwanza kushoto) na Meya Manispaa ya
Singida, Chima Gwae (katikati) wakitiliana saini mkataba wa mradi mkubwa
wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 5.75 za mjini hapa kwa
kiwango cha lami,na mwakilishi wa kampuni ya China Henan Internatioanl
Co operation Ltd ya jijini Dar es salaam, Zephyr Liu. Ujenzi huo
utagharimu zaidi ya shilingi 13.1 bilioni ambazo zimetolewa na benki ya
dunia. (Picha na Nathaniel Limu)
Akifafanua, alisema taratibu za
manunuzi katika mkataba huu zilianza Mei mwaka jana na kukamilika
januari mwaka huu. Ujenzi huo utagharibu zaidi ya shilingi 12.4 bilioni.
“Leo hii Manispaa ya Singida
itatiliana saini mkataba namba LGA/115/SMC/2016/2017 /W/NO.1 na kampuni
ya China Henan International Co-operation Group Co.LTD (CHICO) ya
jijini Dar-es-salaam.Ujenzi huo utakamilika baada ya miezi 12,” alifafanua zaidi.
Mkurugenzi huyo, alisema
CHICO atasimamiwa na kampuni ya Luptan Consultants Ltd ya jijini
Dar-es-salaam kwa gharama ya shilingi 648.3 milioni na itakamilika baada
ya miezi 15.Mkataba wa mradi huo ni LGA/115/SWMC/2016/2017/C/No.02.
“Vile vile tutatekeleza mradi
mwingine wa uandaaji wa mpango mkakati wa miaka mitano wa Manispaa yetu
ya Singida. Mradi huu wenye mkataba LGA/115/SMC/2016/2017/C/No.03 una
thamani ya zaidi ya shilingi 55.9 milioni. Mradi huu utatekelezwa na
mshauri mwelekezi chuo cha mipango Dodoma, Titus Mwageni,” alisema.
Sherehe hiyo ya utiaji saini mikataba
hiyo,zilihudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo na mkuu wa
mkoa wa Singida, Dk.Rehema Nchimbi.
Dk. Nchimbi Alitumia fursa hiyo
kuyaomba mashirika ya TANESCO, TTCL na mamlaka ya maji (SUWASA) kutoa
ushirikiano na mkandarasi ili miundo mbinu yao isikwamishe utekelezaji
wa mradi huo mkubwa ambao utakapokamilika utabadilisha madhari ya mji wa
Singida.
0 maoni:
Chapisha Maoni