SERIKALI ya mkoa
wa Iringa imewaagiza
maofisa ushirika wa
vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) kufanya
uchunguzi na ukaguzi wa
Saccos zote ndani ya wilaya zao
na kuwachukulia hatua kali
viongozi wa Saccos
zitakazobainika kutafuna fedha
za wanachama wake .
Agizo hilo limetolewa
leo na mkuu
wa mkoa wa
Iringa Amina Masenza wakati wa
kikao cha kamati ya ushauri
ya mkoa wa Iringa (RCC)
kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni
Kilimo , alisema kuwa zipo
baadhi ya Saccos ambazo viongozi wake
wametafuna fedha jambo
ambalo halitavumilika .
Hivyo alimwagiza afisa
ushirika wa mkoa wa
Iringa kufanya uchunguzi na
ukaguzi kwa Saccos
zote ili kuzibaini
zile ambazo zimetafuna
fedha za wanachama
wake .
“ Ninakuagiza afisa
ushiriki wa mkoa wa
Iringa fanya ukaguzi Saccos
zote na usiache kuchukua
hatua kali kwa viongozi
ambao watabainika kutafuna
fedha za Saccos”
Katika hatua nyingine
mkuu huyo wa
mkoa aliagiza kuwekwe mkakati wa
kila wilaya wa
kuwalinda watoto wa
kike ambao wamekuwa
wakikatishwa masomo kwa kupewa
mimba na watu
wasiopenda watoto hao
kusoma.
Kauli hiyo ya mkuu
wa mkoa imekuja kufuatia
ushauri uliotolewa na mkuu wa
wilaya ya Kilolo Asia Abdalah
katika kikao hicho
kwa kuomba kikao
hicho kutangaza tatizo la mimba katika
mkoa wa Iringa ni
janga la kimkoa
hivyo kuwekewa mkakati wa
kupambana na janga hilo pamoja na ubakaji watoto .
Akitoa maagizo
kwenye kikao hicho
kufuatia ushauri wa mkuu
huyo wa wilaya ya Kilolo mkuu wa mkoa wa Iringa Masenza alitaka
kila mmoja kwa
nafasi yake kuhakikisha anapambana na mimba kwa
wanafunzi na pia
kuwataka wazazi kuacha mara
moja tabia ya kuwatuma
watoto dukani ama
maeneo mengine usiku .
Huku akiwaomba viongozi
wa dini zote
mkoani Iringa kuendelea kutumia
nyumba zao za
ibada kukemea vitendo vya ubakaji na mimba kwa wanafunzi
huku kwa upande wa jamii inayowazunguka aliitaka
kuacha kuwaficha watu
wanaoendesha vitendo vya ubakaji
na kuarubuni wanafunzi wa
kike .
Katika kikao hicho
mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
aliomba wabunge wote
wanaotoka mkoa wa Iringa
kuungana kupeleka hoja
bungeni ya ucheleweshwaji wa pesa
kutoka serikali kuu
kuja katika Halmashauri .
|
0 maoni:
Chapisha Maoni