VIJANA nchini wametakiwa
kujishughulisha na ufugaji wa nyuki kisha kujikwamua kimaisha kwa kuongeza
kipato, kiuchumi kuliko kutegemea serikali kuwatafutia ajira.
Akizungumza na Mtandao huu wa habari [blog ya KALI YA
HABARI] mapema leo hii ilipomtembelea na kufanya mahojiano maalum kuhusu kilimo
cha asali na changamoto wanazokutana nazo Naibu Mkurugenzi wa TEJO’s Honey,
John Massao ambao niwazalishaji na wasindikaji wa asali asilia mjini Iringa, alisema
kuwa vijana ndio kundi kubwa lisilokuwa na ajira wala mapato katika mfumo wa
maisha na wanahitaji kujiajiri kwa kutumia rasilimali na maliasili zilizoko
katika mazingira yao.
Massao aliwataka vijana hao kujiunga
kwenye vikundi vya pamoja na kuanzisha ufugaji wa nyuki na kuweza kupata asali
na nta kisha kupata soko litakalosaidia kujiinua kiuchumi na kuongeza mapato
katika familia ikiwa ni pamoja na kuepukana na kujihusisha na vitendo vya
uhalifu kwa kuvunja sheria.
Alisema kuwa vijana wasisubiri ajira
za maofisini tu kumbe wange tumia rasilimali ya misitu kufuga nyuki kuliko
kubaki maisha tegemezi na ombaomba kumbe wangeweza kutumia ardhi na misitu ya
asili jirani na hifadhi za Taifa.
“Nchi hii ina mapori mengi lakini
vijana wakijiunga kwa pamoja kwa kuweka mizinga katika mapori ambayo utasaidia
kuhifadhi misitu na mioto,” alisema Massao.
Alisema kuwa asali ikivunwa inadumu
kwa muda mrefu mpaka miaka 100 na haiitaji kupaliliwa wa kuweka mbolea kama
shambani, kwa hiyo vijana watumia fursa waingie katika soko la ufugaji.
Awali Mkurugenzi wa TEJO’s Honey,
Theresia Massao aliitaka serikali na wadau mbalimbali kuhamasisha jamii kufuga
nyuki kwa kutumia njia za kisasa na kuzalisha kwa wingi zao hilo .
Theresia alisema takwimu inaonesha
Tanzania ina misitu mingi ambazo ni makazi ya makundi ya nyuki na ikitumika
vizuri na vijana kufugia nyuki kwa kuzalisha asali itainua kipato cha mwananchi
mmoja mmoja.
“Kutokana na ufugaji wa nyuki jamii
inaweza kujipatia gundi ya nyuki , sumu ya nyuki inayotumika katika tiba pamoja
na maziwa ya nyuki kama chakula na tiba “alisema Theresia.
Vilevile alifafanua kuwa wananchi
kwa kufuga nyuki wataweza kuboresha afya za familia kwa sababu asali inatumika
kama chakula na tiba kwa magonjwa mbalimbali kama vile vidonda vya tumbo na
kansa.
Katika hatua nyingine aliwaasa
wananchi na wafugaji kujiepusha na uharibifu wa mazingira kwa kuchoma na kukata
miti na makazi ya nyuki kwa kukosa maua na maji kisha kuzalisha kiwango kidogo
cha asali na nta na hata kuhama katika mizinga baada ya kupata usumbufu wa
makazi kimazingira.
TEJO ni muuganiko wa majina mawili
yaani, Theresia na John (TEJO) ambao ni mume na mke walieamua kuanzisha kampuni
hiyo baada ya kustaafu utumishi wa umma kama maofisa misitu.
0 maoni:
Chapisha Maoni