Posted by Esta Malibiche on JAN 26,2017 IN MICHEZO
Michezo
miwili ya mwisho ya hatua ya makundi ya michuano ya Afcon 2017
imemalizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana na
hivyo kuongoza kundi D kwa alama 7 huku Ghana wakiwa nafasi ya pili kwa
alama 6.
Bao la
ushindi la mafarao wa Misri lilifugwa na nyota wao Mohamed Salah,
katika dakika ya 11 ya mchezo kwa mkwaju mkali wa mpira wa kutenga
uliokwenda moja kwa moja nyavuni.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo timu ya Uganda walitoshana nguvu na Mali kwa kufungana bao 1-1.
Michezo
ya hatua ya robo fainali itaanza kuchezwa jumamosi ya terehe 28 kwa
Burkina Faso kucheza na Tunisia huku Senega wakicheza na Cameroon.
Jumapili kutacheza michezo miwili ya robo fainali ya pili kwa DR Congo kuchuana na Ghana nao Misri wakipimana ubavu na Morroco.
0 maoni:
Chapisha Maoni