Posted by Esta Malibiche on JAN 16,2017 in NEWS
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKOA
wa Pwani,umekuwa na ongezeko la makosa makubwa 4,208 yaliyoripotiwa
katika mwaka 2016 ambapo makosa ya yaliyochukua nafasi kubwa ni
unyang’anyi wa kutumia nguvu,kupatikana silaha na mauaji.
Ongezeko hilo ni la makosa 419 ukilinganisha na makosa yaliyoripotiwa mwaka 2015 yaliyokuwa 3,784 .
Aidha
makosa madogo 16,332 yaliripotiwa katika kipindi hicho cha mwaka 2016
ambapo kuna ongezeko la makosa 2,396 ikilinganishwa na mwaka 2015
uliokuwa na makosa 13,936.
Akitoa
taarifa ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari,ofisini kwake,kamanda
wa polisi mkoani Pwani Boniventure Mushongi ,alisema ,hali hiyo inawapa
nguvu ya kuongeza kasi ya kupambana/kudhibiti njia za panya na njama
wanazotumia wahalifu.
Hata
hivyo alieleza,katika kipindi cha Jan hadi desemba 2016 ,kumekuwepo na
baadhi ya matukio yaliyovuta hisia za watu ikiwemo tukio kupatikana kwa
miili ya watu saba kwa nyakati tofauti wilayani Bagamoyo.
Alitaja
matukio mengine ni yaliyosababisha vifo vya viongozi wa serikali za za
vijiji kwa Mkuranga ,Rufiji na Kibiti ambapo watu 11 walikamatwa na
wameshafikishwa mahakamani.
Mushongi
alisema kati ya makosa yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi ni pamoja
na unyang’anyi wa kutumia nguvu makosa 294 ukilinganisha na makosa 197
yaliyoripotiwa 2015 hivyo kuwa na ongezekjo la makosa 57.
Makosa
mengine ni kupatikana kwa silaha makosa 25 ambapo 2015 yalikuwa 20
ongezeko 5 na makosa ya mauaji kwa mwaka 2016 ni 126 huku 2015 yakiwa
107 tofauti 19.
Makosa
mengine ni unyang’anyi wa kutumia silaha ,uvunjaji,magendo makosa 52,na
makosa ya kubaka yameongezeka kutoka 340 hadi kufikia 416 mwaka 2016.
Mushongi
alieleza kuwa,ongezeko la makosa hayo imetokana na misako iliyofanywa,
doria na oparesheni zilizokuwa zikifanywa kwenye maeneo mbalimbali na
kushirikisha jamii.
“Tunawashukuru
wananchi ,wasamaria wema,kwa ushirikainao wao na jeshi letu,tunawaomba
waendelee na ushirikiano huo wa kutoa taarifa mbalimbali ambazo
zinasaidia kukabiliana na uhalifu “
“Uwiano
wa askari na raia bado hautoshi kwani askari mmoja anahudumia raia
zaidi 1,000 hivyo ulinzi shirikishi ni muhimu ndani ya jamii,” alisema
Mushongi.
Alisema
katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita walifikisha mahakamani makosa
1,439 sambamba na hilo watuhumiwa wa makosa 159 walikutwa na hatia na
kuhukumiwa kifungo wakati makosa 29 watuhumiwa walishindwa kutiwa
hatiani na kuachiwa huru.
Jeshi
hilo licha ya kukabiliana na wahalifu mbalimbali lakini linakabiliwa na
changamoto ya upungufu wa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na uchache wa
magari,Jiografia ya mkoa kwenye mipango miji ni ngumu kumpata mhalifu
kwa haraka pindi uhalifu unapotokea.
Muingiliano
na mkoa wa Dar es Salaam unafanya wahalifu kuweza kuingia kirahisi na
kufanya makosa na uuwepo wa ukanda wa mkubwa katika bahari unaosababisha
kuwepo kwa bandari bubu nyingi za kupitisha wahamiaji haramu na
biashara za magendo.
0 maoni:
Chapisha Maoni