Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
akipatiwa maelezo na Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret
Mlyomi (katikati), wakati alipofika katika ziara ya kushtukiza kwenye
Ofisi za Shirika la Posta, Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo kuangalia
shughili mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo.
Mkuu
wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe
(kushoto), akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarwa kuhusu mambo ya
usalama kwenye mtandao wa shirika hilo. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa
Shirika la Posta, shughuli za biashara, Janeth Msofe.
Waziri
Profesa Mbarwa, akimsikiliza mteja wa shirika hilo, Mhandisi Nungu
Allanus kutoka DIT, kuhusu ubora wa utoaji huduma wa shirika.
Waziri
Profesa Mbarwa (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Msaidizi Meneja
wa Fedha na Huduma wa shirika hilo, wakati alipotembelea kitengo kipya
cha kutolea huduma mbambali za kifedha cha Jamii Centre. Katika
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dk. Harun Kondo.
Waziri
Profesa Mbarwa (kushoto), akimweleza jambo Meneja wa Posta Mkoa wa Dar
es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati akitembelea Posta Kuu,
maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ziara hiyo.
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania,
George Mwamgabe.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (katikati), akimweleza
jambo Waziri Profesa Mbarawa, akitembelea vitengo mbalimbali vya Ofisi
za Posta Kuu jijijini katika ziara hiyo.
Kaimu
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga,
akizungumza wakati Waziri Profesa Mbarawa alipokutana na wafanyakazi na
kuzungumza nao Makao Makuu ya shirika hilo, wakati akimaliza ziara yake
hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (kulia),
akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa Mbarawa, kuzungumza na wafanyakazi, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati
wa kumaliza ziara yake hiyo.
Waziri Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati
wa ziara yake hiyo.
Ofisa
Mwandamizi wa Shirika la Posta, Makao Makuu, David Hango, akizungumza
wakati akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya changamoto
zinazolikabili na kukwamisha shirika hilo katika kupiga hatua za
kimaendeleo.
Mmoja
wa wafanyakazi wa shirika hilo kutoka Chama cha Wafanyakazi cha Tewuta,
Ahmed Kaumo, akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya
changamoto ambazo angependa kuwa na kikao cha pamoja cha Viongozi wa
shirika hilo na wa chama hicho cha wafanyakazi katika kukabiliana nazo
ili kulikwamua shirika hilo.
Mmoja
wa wafanyakazi wa shirika hilo, upande wa Masoko, Joyce Kagose,
akimweleza Waziri Profesa Mbarawa changamoto mbalimbali zinazolikabili
shirika hilo.
Mmoja
wa wafanyakazi wa zamani wa shirika hilo, akimweleza kwa uchungu Waziri
Profesa Mbarawa jinsi changamoto wanazozipata kutoka kwa baadhi ya
watendaji wa shirika hilo, ambao hujifanya wasomi na kuwazarau wale wa
zamani kutokana na elimu zao.
Waziri Profesa Makame Mbarawa (katikati), akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na wafanyakazi hao.
Waziri Profesa Makame Mbarawa, akijibu baadhi ya hoja na ushauri wa wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa ziara yake hiyo.(Picha zote na Kassim Mbarouk
0 maoni:
Chapisha Maoni