Posted by Esta Malibiche on JAN 18,2017 IN NEWS
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto mbele)
akibadilishana mawazo na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya
Nishati na Madini kwenye ziara ya kuelekea katika kisiwa cha Ukara
wilayani Ukerewe, Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua
inayotekelezwa na kampuni ya Jumeme Rural Power Supply.
Sehemu ya kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme Rural Power Supply kilichopo Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Jumeme Rural
Power Supply, Sitta Ngissa (katikati) akielezea hali ya uzalishaji umeme
kwa kutumia nishati ya jua katika kituo hicho, Kushoto ni David
Mwakigonja kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Mfumo wa kuongozea mitambo na vifaa vya
kuzalisha umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme
Rural Power Supply
Mtaalam kutoka kampuni ya Jumeme Rural
Power Supply, Mhandisi Egberth Bashuweka (kulia) akifafanua jambo kwa
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto)
Mtaalam kutoka kampuni ya Jumeme Rural
Power Supply, Mhandisi Egberth Bashuweka (kushoto) akieleza jambo katika
chumba cha betri kwa ajili ya kuhifadhi umeme kwa Kamishna Msaidizi-
Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden
Rwebangila (kulia)
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (katikati
mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati,
Wizara ya Nishati na Madini na watendaji kutoka kampuni ya Jumeme Rural
Power Supply.
Mtaalam kutoka kampuni ya Jumeme Rural
Power Supply, Mhandisi Egberth Bashuweka (kulia) akielezea kazi ya mita
za umeme jua kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto).
……………….
Na Greyson Mwase, Mwanza
Wananchi wa wilaya ya Ukerewe wameipongeza
serikali kwa kasi ya miradi ya umeme katika wilaya hiyo, na kuongeza
kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea ukuaji wa shughuli za
kiuchumi hususan za uvuvi.
Waliyasema hayo katika nyakati tofauti
jana katika ziara ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara
ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na wataalam
kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini yenye lengo la
kujionea hatua iliyofikiwa ya maendeleo ya miradi hiyo inayotekelezwa na
kampuni ya Rex Energy
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Katibu wa
Kitongoji cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe, Frank Matondane alisema
kuwa kitongoji hicho hakikuwa na ndoto ya kupata umeme wangu
kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika lakini matumaini yamepatikana baada
ya kuanza kwa utekelezaji wa miradi ya umeme katika kitongoji hicho
kupitia kampuni ya Rex Energy.
Alisema mara baada ya wananchi
kuhamasishwa na wataalam kutoka kampuni ya Rex Energy na kuona zoezi la
ujenzi wa miundombinu ya umeme, walitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja
na kutodai fidia hali iliyorahisisha utekelezaji wa mradi huo.
Matondane alisema kuwa mahitaji ya umeme
katika kitongoji cha Ghana/Siza chenye wakazi wanaokadiriwa kuwa kati
ya 2,500 hadi 5,000 ni makubwa husuan wavuvi wanaohitaji umeme kwa
ajili ya kwenye majokofu ya kuhifadhia samaki.
Aliongeza kuwa shule pamoja na maduka ya
madawa baridi yanahitaji umeme na kusisitiza kuwa mara baada ya
kukamilika kwa mradi huo, uchumi katika kisiwa hicho utakua kwa kasi
kutokana na fursa zilizopo na kuvutia wawekezaji kwenye ujenzi wa
kiwanda cha kusindika nyama ya samaki.
Naye mmoja wa wakazi wa kitongoji hicho,
Emanuel Mfungo alisema kuwa wakazi wa kitongoji hicho wameshaanza
kuweka mifumo ya umeme kwenye nyumba zao kwa ajili ya kujiandaa na
huduma ya kuunganishwa na huduma ya umeme.
Alisema kuwa kutokana na kutambua umuhimu
wa umeme, wananchi wa kitongoji hicho weamekuwa ni walinzi wa
miundombinu ya umeme ili kutohujumiwa na watu wasiotakia mema kitongoji
hicho.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji
kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa akielezea hatua
iliyofikiwa ya mradi huo, alisema kuwa kazi ya ujenzi wa miundombinu
imeshakamilika katika kituo chote na kusisitiza kuwa kampuni inatarajia
kufunga mtambo wa kuzalisha umeme kwa umeme jua wenye uwezo wa Kilowati
350 ambapo utaongezwa uwezo wake kutokana na mahitaji ya umeme katika
kitongoji hicho.
0 maoni:
Chapisha Maoni