Posted by Esta Malibiche on JAN31,2017 IN NEWS
Mwenyekiti
wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha
Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,
Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar
es Salaam juzi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO
BLOG)
Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah
Na Richard Mwaikenda
MJUMBE
wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah,
amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa
kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.
Anna
Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo
wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.
Alisema
ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA
wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi
bora wa baadaye.
Anna
Abdalla alisema kuwa hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya
viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za
usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri.
Pia
katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake
na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara kukutana na wasichana
kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na
hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.
"Nataka
siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu
Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje
mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike,
ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge,
Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi
na waalikwa katika hafla hiyo.
Katika
hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya
Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo
pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo
nchini
katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni;
Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na
Andriambolamanana Vahatrimama.
Kamishna
Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa
ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Sophia Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa
Bodi hiyo atateuliwa miongoni mwao.
Mwenyekiti
wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha
Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA, Anna
Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es
Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema
(aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA
wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa ambaye ni
Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna
Mkuu wa TGGA, Hangi.
Wasichana
Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda),
katikati, na Andriambolamanana Vahatrimama wa Madagascar ambao wapo
nchini kaitika programu ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika
masuala ya utamaduni, uongozi na maadili.wakiwa katika hafla hiyo.
Wakipiga makofu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Anna Abdalah
Anna Abdalah akihutubia katika hafla hiyo
Mmoja wa wabia wa moja kati ya majengo ya TGGA, akisalimiana na Anna Abdalah
Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shebe akitoa shukrani kwa wajumbe wapya wa bodi na wageni waalikwa kwa kuhudhuria uzinduzi huo.
Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA pamoja na wanachama wa chama hicho.
Sasa ni wakati wa msosi
Wajumbe wa Bodi wakijadiliana jambo na watendaji wa TGGA
Profesa Qooro akimuaga Zakia Meghji. Katikati ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
Qooro akigana na Anna Abdalah. Kushoto ni Hangi
Mjumbe wa Bodi Grace Makenya akiaga |
0 maoni:
Chapisha Maoni