Posted by
Naibu Waziri Tamisemi,Seleman Jafo
Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
NAIBU Waziri
Tamisemi ,Selemani Jafo amemtaka afisa Uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya
Mafia,mkoani Pwani kuhakikisha anadhibiti uvuvi haramu wa kutumia
mabomu na kama uvuvi huo utaendelezwa afisa huyo atawajibishwa.
Sambamba na
hayo ameeleza halmashauri ya wilaya ya Mafia hali sio shwari hivyo
watendaji wajitume kwa kufuata kasi ya serikali iliyopo madarakani.
Alisema,
matumizi ya mabomu yamekua mwiba kwa mazalia ya samaki baharini ambayo
madhara yake ni makubwa kwa nyakati zijazo ambayo yanatakiwa kudhibitiwa
mapema.
"Nikisikia
uvuvi haramu wa kutumia mabomu unaendelea huku samaki wakifa na
kupunguza ongezeko, afisa uvuvi kazi hana, kwasababu tunaendelea kutoa
maagizo lakini hakuna usimamizi mzuri"alisema Jafo.
Alisema, uvuvi haramu matumizi ya mlipuko na nyavu hazistahili kutumika katika kuvua samaki na ni jambo la hatari.
Aliwataka watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani baadhi ya mambo yanaendelea kuzorota kwa kutokua na mabadiliko.
Jafo alisema, athari kubwa itakua kwa kwa watu ambao watashindwa kufuata maelekezo ya viongozi.
Aidha alisema
Halmashauri ya wilaya ya Mafia bado hali si nzuri kutokana na utendaji
mbovu na kama wapo watendaji wataendelea kutowajibika na kubadilika
hatua zitachukulia.
0 maoni:
Chapisha Maoni