Postedy by Esta Malibiche on JAN 30,2017 IN SIASA
|
CHAMA cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa kimezindua sherehe za miaka 40 tangu kuzaliwa kwake mwaka februari 5,1977.
Sherehe
hizo zilifanyika katika Manispaa ya Iringa na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali.
Chama cha Mapinduzi ccm huadhimisha kila mwaka kuzaliwa kwake,ambapo kwa mwaka 2017 zitafanyika Mkoani Dodoma februari 5.
Akizungumza katika sherehe hizo, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu aliwataka wanaccm kukienzi chama kwa vitendo kwa kufuata
nyayo za waasisi.
''Ninawashukuru waasisi wa ccm kuanzia TANU ,Tanzania bara na Zanzibar ,kwasababu waliweza kukitetea chama na kuweka misingi
imara hadi hivi sasa kinaendelea kushika atamu''''alisema Msambatavangu
''Ingawa tuko katika mfumo wa vyma vingi lakini tunaendelea kupambana na kuhakikisha ccm inashika dora''
Awali
katibu wa ccm Iringa Mjini Nuru Ngereja alisoma Historia ya ccm tangu
kuanzishwa kwke na kusema kuwa Chama cha Mapinduzi ccm kilizaliwa
tarehe 5,februari 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika
African Union [TANU] na Afro- Shirazi Part [ASP]
Ngereja
alisema Muungano wa TANU na ASP ndio uliowezesha CCM kuwa chama chenye
nguvu, imara na madhubuti.Hivyo chama cha siasa chenye uwezo wa hali ya
juu ya kuwaunganisha watanzania.
''''''Poamoja na kwamba Chama cha Mapinduzi kuwa kilizaliwa rasmi tarehe
5 februari,1977,chimbuko lake linaanzia miak mingi kabla,sambama na
historia ya uhai wa Taifa la Tanzania.Mzizi ya CCM ya Historia ya CCM
imo ndani ya harakati za kukaa ukoloni na usultani,zilizofanyika na
wananchi wa Tanzania '''alisema Ngereja |
|
|
|
|
|
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akizungumza katika sherehe ya uzinduzi wa 40 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi zilizofanyika Jumamosi 28,1.2017
0 maoni:
Chapisha Maoni