Posted by Esta Malibiche on JAN 16,2017 in NEWS
Mkuu
wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza na watumishi wa
Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhusu ubadhilifu uliofanyika wakati wa
zoezi la utengenezaji wa madawati.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri
hiyo Yahana Sintoo.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akionesha sehemu ya nyaraka
ambazo zinaonesha namna baadhi ya watumishi walivyoshiriki kufanya
ubadhilifu wa fedha za madawati.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanawa (katikati) akiwa na katibu
tawala wa wilaya hiyo,Upendo Wela (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa
Halamshauri ya wilaya hiyo Yohana Sintoo (kushoto).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungungunza wakati wa kikao hicho .
Na Dixon Busagaga,Hai.
MKUU
wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ametoa jukumu kwa mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya hiyo,Yohana Sintoo la kuamua hatma ya watumishi
wake watano wanaotajwa katika tuhuma za ubadhilifu wa fedha wakati wa
zoezi la utengenezaji wa madawati.
Akiwa
ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa halmashauri hiyo,Mkurugenzi
Sintoo ndiye mwenye maamuzi ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya
tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya hiyo, Byakanwa kumaliza kazi yake ya
uchunguzi dhidi ya watumishi hao na kubaini mapungufu kadhaa.
Akihitimisha
taarifa yake wakati wa kikao na watumishi wa halmashauri hiyo,Byakanwa
aliagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza
na kuchukua hatua dhidi ya watumishi hao akiwemo aliyekuwa kaimu
Mkurugenzi ,Mhandisi Kweka.
“Mamlaka
ya nidhamu ya watumishi wa Halmashauri ni mkurugenzi pamoja na baraza
la madiwani ,lakini mwajiri ni ofisi ya katibu tawala mkoa ,Ofisi hizi
mbili ndizo zinazoweza kukaa na kuchukua hatua za kuzuia matukio au
vitendo kama hivyo.”alisema Byakanwa.
“Niishauri
ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ambayo ndio mamlaka ya
nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya
watumishi hawa”aliongeza Byakanwa.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema tuhuma zinazowakabili watumishi hao ,majina yao
tumeyahifadhi kwa sasa ni pamoja na kupitisha barua ya malipo bila
kujiridhisha kama kuna mkataba wa kutengeneza madawati na kufanya malipo
ya fremu za madawati badala ya madawati.
Tuhuma
nyingine inaihusu timu ya ukaguzi iliyokiri kukamilika kwa kazi bila
ya kuonesha kama walipokea madawati au walienda kukagua kazi ya mzabuni
licha ya mzabuni kuomba malipo ya fremu za madawati badala ya Madawati
kamili.
Ofisi
ya elimu msingi,ofisi ya mkurugenzi,ofisi ya Mhasibu wa Halamshauri na
kitengo cha manunuzi pia zinatuhumiwa kushindwa kubaini nyaraka
zilizowasilishwa na mzabuni endapo zilikuwa ni kwa ajili ya fremu za
Madawati badala ya Madawati kamili.
Katika
kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Byakanwa alisema kampuni iliyopewa zabuni ya kutengeneza madawati ni ya
Ujenzi na haijawahi kufanya kazi ya kutengeneza madawati, kuwa na
karakana wala vifaa vya uselemala .
Byakanwa
alisema kwa malipo yaliyofanyika Halmashauri ilipoteza zaidi ya sh Mil
12 huku akishangazwa na hatua ya mmoja wa watumishi wanaotuhumiwa kuomba
malipo badala ya mzabuni.
Akionyesha
namna watumishi hao walivyokiuka taratibu Byakanwa alisema taarifa ya
uchunguzi inaonyesha Halmashauri iliunda timu ya ukaguzi ambayo katika
cheti cha ukaguzi na mapokezi ya bidhaa kinaonyesha bidhaa au madawati
yalipelekwa ,Julai 16, 2016 ,siku 12 tangu siku ya mkataba na mzabuni.
“Mmoja
w wajumbe wa kamati hiyo ya ukaguzi alikuwa ni mjumbe wa kamati ya
kuratibu zoezi la Madawati ,alikuwa na jukumu la kusambaza mbao kwa
wazabuni na alikuwa anajua kuwa hajapeleka mbao za kutosha kwa mzabuni
,katika maelezo yake mbele ya tume anakiri kuwa mzabuni hajamaliza kazi
kwa sababu Halmashauri haijampa mbao.”alisema Byakanwa.
Alisema
mzabuni aliieleza tume kuwa anadaiwa madawati 246 na halmashauri na
kuwa amekamilisha kutegeneza madawati 154 na ueleza kua alishindwa
kukamilisha kutokana na kukosa mbao kutoka halmashauri.
“June
9,2016 malipo ya Sh Mil 19.2 yakalipwa kwa ajili ya fremu za madawati
siyo Madawati.Vocha ya malipo ikasainiwa na DT na kuandaliwa na mtumishi
mwingine (jina tunalo) ikakamilisha mchezo.”alisema Byakanwa.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kufanya hivyo ilikuwa ni kinyume cha taratibu za
malipo kwa kuwa wahusika walipaswa kujiridhisha na nyaraka walizokuwa
wakitumia ,kwa nini mzabuni aliamua kudanganya Halmashauri.
Byakanwa
aliishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi
ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ambayo ndio mamlaka ya
nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya
watumishi hao.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yahana Sintoo
alisema licha ya kwamba amefika wakati zoezi la uchunguzi lina kamilika
bado atafanyia kazi taarifa hizo kwa umakini mkubwa ili kujiridhisha na
utendajji kazi wa watumishi wa halmashauri hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni