Katika kipindi cha
miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016,
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa
na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama
hicho mwaka wa fedha 2015/16.
Ukusanyaji wa mapato
katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia
12.74. Mlinganisho wa makusanyo
ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
MWEZI
|
MWAKA 2015/16
|
MWAKA 2016/17
|
Ongezeko
|
JULAI
|
925,384.7
|
1,069,458.5
|
15.57
|
AGOSTI
|
923,316.9
|
1,154.222.5
|
25.01
|
SEPTEMBA
|
1,132,310.3
|
1,378,048.9
|
21.70
|
OKTOBA
|
1,037,179.8
|
1,131,094.9
|
9.05
|
NOVEMBA
|
1,027, 939.6
|
1,123,509.7
|
9.30
|
DISEMBA
|
1,403, 189.8
|
1,414,921.8
|
0.84
|
JUMLA
|
6,449,321.1
|
7,271,256.26
|
12.74
|
Jitihada mbalimbali
zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika
ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya
ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba
mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine
za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.
TRA inaendelea
kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama
ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.
Pamoja na hayo
tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya
uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa
zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika
mikoa mingine.
TRA inatoa wito kwa
wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate
mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
Kwa wafanyabiashara
wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na
Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.
Wamiliki wa majengo
wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari.
‘Pamoja Tunajenga
Taifa Letu’
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA
NA ELIMU KWA MLIPAKODI
0 maoni:
Chapisha Maoni