Posted by Esta Malibiche on JAN 30,2017 IN NEWS
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa habari jana mjini
Dodoma, kuhusiana na uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya
Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga,
kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali
inayochangia kukausha vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti.
Kundi la mifugo likiwa ndani ya Pori Tengefu la Loliondo, karibu kabisa na mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii inalaani vikali uchochezi unaofanywa na Mashirika
yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi
kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo
hali inayochangia kukausha vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti.
Akizungumza na Waandishi wa habari
jana mjini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne
Maghembe amesema maelfu ya mifugo kutoka nchi jirani ya Kenya imekuwa
ikiingizwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti muda wa saa 11 jioni,
Amesema katika kukabiliana na
changamoto ya uharibu wa chanzo kikuu cha maji ya Serengeti kwa asilimia
47.2 ya maji yote, tayari mifugo 1700 imeshakamatwa
Mbali na mifugo hiyo, Waziri
Maghembe alisema kuwa maelfu ya Matrekta ya kutoka nchini Kenya
yameletwa kulima katika maeneo yanayopakana na Serengeti
Aliongeza kuwa hivi karibuni
kilimo kimeshamiri ambapo kipindi cha nyuma wakazi walikuwa wanalima na
ng’ombe (maksai) ila sasa matrekta ya Kenya yanalima na kufungua
mashamba makubwa.
Kufuatia hali hiyo, Waziri
Maghembe ameagiza kuwa raia wa Kenya wenye mifugo Loliondo warudi
makwao mara moja, Mkoa na Wilaya uchukue hatua kuwaondoa mara moja
Pia, Matrekta yote ya nchi ya Kenya yawe na usajili wa kodi (Tax Clearance) toka TRA au yarudi kwao mara moja
Aidha, ameagiza kuwa eneo la 1,5002km liwekewe alama mara moja na uwekaji alama ukamilike ifikapo tarehe 30 Machi, 2017.
Kwa upande wa Utalii, Ameziagiza
kampuni zote za utalii ambazo hazina usajili wa kitaifa zinazofanya
biashara kwa mikataba ya vijiji ziripoti Wizarani ndani ya siku saba,
Ikiwa pamoja na kuonyesha usajili wao, kuonyesha vitalu walivyopewa na
Serikali pamoja kuiridhisha Serikali kama wanalipa kodi.
Awali, akizungumzia kuhusu mgogoro
huo wa Pori Tengefu la Loliondo, Waziri Maghemba alisema anatambua kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anasimamia mazungumzo ya wadau
wote ili kuleta utatuzi wa mgogoro huo.
‘’Nimeambiwa kuwa mwelekeo wa
mazungumzo ni mzuri nahimiza mazungumzo yaendelee, lakini nimeona
nikingoja hadi mazungumzo hayo yaishe Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
itakuwa haipo.’’ alisisitiza
0 maoni:
Chapisha Maoni