Posted by Esta Malibiche on JAN30,2017 IN NEWS
Na. Ahmad Mmowa, Lindi
Utafiti
uliofanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara (kanda ya kusini)
umesababisha kugunduliwa kwa mashapo ya madini aina ya bunyu (kinywe)
yenye uzito wa tani 689.7 milioni
Hayo
yameelezwa na mhandisi wa migodi wa kanda ya kusini, Aidan Mhando
kwenye kongangamano la siku moja la wadau wa mradi wa uchimbaji wa
madini ya bunyu katika vijiji vya Namangale, Utimbula vilivyo katika
wilaya Lindi na mkoa wa Lindi, Chidya na Chiwata vilivyopo katika
wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara. Yaliyofanyika katika manispaa ya Lindi.
Mhandisi
Mhando ambae pia ni kaimu kamishna msaidizi wa madini wa kanda ya
kusini, alisema kazi ya kuchimba kiasi hicho kilichogunduliwa inakaribia
kuanza hivi karibuni.
Kwasababu
hatua iliyobaki ni kupata leseni ya uchimbaji baada ya hatua nyingine
kukamilika. Aliyataja maeneo ambayo uchimbaji huo utafanyika kuwa ni
Namangale, Utimbula, Chiwata na Chidya. Ambapo mitambo mikubwa ya
kuchakata itajengwa katika vijiji vya Utimbula na Namangale vilivyopo
katika wilaya ya Lindi. Kutokana na uwingi wa madini hayo katika vijiji
hivyo.
Alisema
soko la bunyu ni zuri na kubwa kutokana na kuzalishwa na nchi chache
wakati mahitaji ni makubwa. Akibainisha kwamba wazalishaji wakubwa
walikuwa ni nchi ya China. Hata hivyo hivi sasa nchi hiyo haizalishi kwa
wingi.
"Kuna
haja ya kuanza uchimbaji haraka ili kuwahi soko kutokana na baadhi ya
nchi jirani, ikiwamo Msumbiji inatani takribani bilioni mbili za madini
hayo," alisema Mhando.
Mhandisi
Mhando alizitaja kampuni za kampuni za utafiti ziligundua madini hayo
kuwa ni Urinex inyofanya utafiti katika wilaya ya Ruangwa iliyogundua
mashapo yenye uzito wa tani 174 milioni, Nachi katika wilaya ya Lindi
(tani milioni 446), Lindi jumbo (tani milioni29.6) katika wilaya ya
Ruangwa, na Ngwena (tani milioni 25) katika wilaya Ruangwa na
Nachingwea.
Mhando alibainisha kuwa kampuni nyingine zinaendelea kufanya utafiti katika wilaya za Nachingwea na Ruangwa.
Huku akizitaja kampuni hizo kuwa ni Nazareti, Pacco na ASA.
Aidha
kaimu kamishna huyo alisema hadi sasa zimeshatolewa leseni ndogo za
utafiti 4183 katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Ambapo katika mkoa wa
Lindi zimetolewa 3625, na Mtwara 558.
Nae
mwakilishi wa kampuni ya Nachi, mhamdisi Jimmy Ijumba alisema kampuni
hiyo ambayo itachimba madini hayo inatarajia kusafirisha tani 100,000
hadi 180,000 kwa mwaka.
Ijumba
alizitaja baadhi ya faida zitakazo patikana kupitia mradi huo pindi
uchimbaji utakapoanza kampuni hiyo itawaajiri watu 270. Ambapo watu 220
kati ya hao watakuwa wazawa.
"Mradi
utakuwa na faida nyingine, ikiwa ni pamoja na kuvutia uwekezaji mwingi
wa huduma na uzalishaji mali ambao utapelekea utengenezaji wa fursa na
ajira zaidi kwa wakazi wa maeneo ya mradi," alisema Ijumba.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Masasi, Semani Mzee alitoa wito kwa
wawekezaji. Ikiwamo kampuni ya Nachi watumie uzoefu wa utekelezaji wa
miradi iliyofanyika ili kuepuka kuwa chanzo cha migogoro kutokana
kutolipa fidia kwa wakati kwa wanachi wanaachia maeneo na mali zao kwa
ajili ya kupisha miradi mbalimbali.
Ambapo
pia alitoa wito kwa wananchi wenye tabia ya kuendeleza maeneo ambayo
yameshafanyiwa tathimini kwa lengo la kulipwa fidia kubwa waache tabia
hiyo.
Kongamano
hilo lililokuwa na lengo kuwajengea uelewa wadau hao kuhusu mradi huo
uliwashirikisha pia wawakilishi kutoka kata za Chiwata na Namangale na
viongozi wa serikali za vijiji vya Utimbula, Namangale A na B.
0 maoni:
Chapisha Maoni